Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

“The ENTITLED” Aina ya watu ambao unatakiwa kuwa nao makini…
Kama wewe ni mmoja wao unatakiwa kufanya bidii za kubadilika.
Watu wa aina hii huwa na sifa kuu tatu:
1. Huwa wanaona kuwa wewe una wajibu wa kuwasaidia kila wanapokuwa na shida.
Mara nyingi watu hawa wanataka kila wanapokuomba kitu chochote hata kama ni msaada lakini huwa kama WANAKULAZIMISHA.
Ukiwaambia hauna wanaanza kulalamika na kumwambia kila mtu kuwa HAUJAWASAIDIA.
Hii hutokea hata kama umeshawahi kuwasaidia mara nyingi ila ukashindwa mara moja tu.
2. Huwa wanaamini kuwa kila wakati unatakiwa USITISHE VIPAUMBELE VYAKO ili ushughulikie changamoto zao.
Wakikuambia changamoto yao wanataka uache kila Kitu uanze kushughulikia matatizo yao.
Ukiwaambia umebanwa au kuna kitu cha muhimu unakifanya wakati huo, wanaanza kusema hauwajali na hauwapendi.
Hawako tayari kusikiliza na kujua changamoto unazozipitia kwa upande wako.
Watu hivi anaweza asikutafute kabisa lakini siku ukimtafuta…
Cha kwanza ni kulaumu “siku hizi haunitafuti” wakati hata yeye hajawahi kukutafuta.
Huwa wanaamini wewe ndio una wajibu wa kuwatafuta na sio wao.
3. Huwa wakija kwako wanatumia neno “NIAZIME” ama “NIKOPESHE”…
Lakini cha kushangaza ukishawapa hawajishughulishi kabisa kukulipa na wanakuwa wasumbufu.
Hata unapoonyesha kuwa unahitaji kwa haraka wao watakuwa wanachukulia poa tu.
Yaani hawa ukiwakopesha au kuwaazima kitu huwa wanachukulia kama umewapa na HAWAONI WAJIBU wa kurudisha.
Ukiwa na mtu wa namna hii jitahidi kuwambia ukweli…
Ingawa wengi wana TABIA ya KUSUSA na KUKASIRIKA HARAKA, ila hakuna namna.
Na kingine jitahidi kujiepusha kuwaazima vitu/pesa kiwango ambacho hauko tayari kuipoteza.
Je, kuna yoyote unayemfahamu mwenye sifa hizi?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.