Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuwa na ndoto kubwa sio ishu kubwa sana, kila mtu anaweza kuwa nayo….
Tofauti huanzia kwenye mtazamo na bidii ya kuanza kufuatilia ndoto tulizonazo.
Kanuni ya 40+ (Forty Plus) inasema kuwa, mtu anayefanya kazi masaa 40 kwa wiki (wastani wa masaa 8 kwa siku)…
Hayuko kwenye safari ya kujenga mafanikio makubwa bali kwenye safari ya kupata mahitaji muhimu ya kila siku tu.
Jitahidi wiki Mpya inapoanza kujiuliza mbinu unazoweza kutumia kuongeza muda wa kufanyia kazi ndoto zako.
Kama umeajiriwa jitahidi upate siku kadhaa ambazo unatoka wakati mzuri kazini kwako na unatumia muda huo kufukuzia ndoto zako.
UKUBWA wa MANENO NA MALENGO yako Unatakiwa ufanane na UKUBWA WA BIDII ZAKO.
Punguza masaa ya Kulala, ongeza muda wa kufanyia kazi ndoto zako.
Punguza Muda wa Kuangalia TV, Tumia kusoma vitabu.
Punguza tamthilia na mechi za kuangalia, tumia muda huo kufanya vitu vya kukuongezea thamani.
NISHIRIKISHE WIKI HII UNAPANGA KUFANYA NINI KATIKA KUTIMIZA MALENGO YAKO?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.