Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahakama ya China imewahukumu kifo watu 11 wa familia yenye sifa mbaya iliyokuwa ikiendesha vituo vya utapeli nchini Myanmar, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya China.
Makumi ya jamaa wa familia ya Ming walipatikana na hatia ya kufanya vitendo vya uhalifu, huku wengi wakipokea vifungo vya muda mrefu gerezani.
Familia ya Ming ilifanya kazi katika moja ya koo nne zilizoendesha mji wa Laukkai, karibu na mpaka wa Myanmar, na kuugeuza kuwa kitovu cha kamari, dawa za kulevya na vituo vya utapeli.
Hatimaye Myanmar ilichukua hatua na kuwakamata watu wengi wa familia hizo mwaka wa 2023 na kuwakabidhi kwa mamlaka ya China.
Jumla ya wanafamilia 39 wa Ming walihukumiwa siku ya Jumatatu katika mji wa mashariki wa Wenzhou, kulingana na ripoti ya shirika la utangazaji la serikali ya China CCTV.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.