“You don’t have what it takes to be a Musician”-Louis Armstrong

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Louis Armstrong alikuwa ni mmoja wa wanamuziki wa Jazz waliofanikiwa sana…

Hata hivyo kuna siku alielezea kisa chake kimoja ambacho kina mafunzo makubwa sana ndani yake.

Wakati ameanza kutamani kuimba aliwahi kujiandikisha ili aonyeshe uwezo wake ili apate nafasi (audition).

Siku alipokwenda alijikuta ameweza kuimba “note” mbili tu za kwanza vizuri na zilizobakia alishindwa.

Mmoja wa majaji akamwambia “You don’t have what it takes to be a Musician”

Akimaanisha kuwa hakuwa na uwezo wa kuwa Mwanamuziki.

Anasema baada ya hapo alirudi nyumbani na alilia sana kwa sababu ya kukataliwa.

Baada ya Muda akamwita rafiki yake akamwambia…

“I know there’s music in me, they can’t keep it out” (Najua kuna muziki ndani yangu na hawawezi kuuzima).

Akaendelea kufanya bidii hadi akaja kuwa mwanamuziki mkubwa wa Jazz.

Kuna watu wengi wana vitu vikubwa ndani yao ila wameruhusu wengine wavizime na wameshakata tamaa.

Inawezekana kuna mtu amekuambia hautaweza kuwa unavyotaka, USIKUBALI wazime Ndoto Yako.

Kuna watu wengi sana ambao HAWAJUI ulichonacho ndani yako…

Hawajui uwezo uliojificha ndani yako, hawajui nguvu uliyobeba…

USIRUHUSU VIGEZO vyao JUU YAKO, VIZIME NDOTO KUBWA ULIYOBEBA.

Leo kwa mara nyingine jiambie “Wamenikataa kwa sababu hawajui kilichopo ndani yangu, sitakata tamaa”.

Je, unaiamini ndoto yako kama Armstrong hata kama wengine hawataki kuiamini?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment