Trump asema Ukraine inaweza kuyakomboa maeneo yake yote yaliyotekwa na Urusi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani anasema Ukraine inaweza kukoyamboa maeneo yake yote yanayodhibitiwa na Urusi kwa kuunga mkono na Nato na Ulaya, na kuashiria mabadiliko makubwa katika msimamo wake.

Trump asema Ukraine inaweza kuyakomboa maeneo yake yote yaliyotekwa na Urusi

v

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Kyiv inaweza “kushinda Ukraine yote na kuirejesha katika hali yake awali”, na hivyo kuashiria mabadiliko makubwa katika msimamo wake kuhusu vita na Urusi.

Katika chapisho kwenye jukwaa lake la la kijamii, Truth Social , amesema Ukraine inaweza kurudisha “mipaka ya asili kutoka mahali ambapo vita hivi vilianza” kwa msaada wa Ulaya na Nato, kutokana na shinikizo kwa uchumi wa Urusi.

Maoni yake yamekuja baada ya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, yaliyofanyika baada ya Trump kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumanne.

Trump amerudia kuelezea nia yake ya kumaliza vita, lakini hapo awali alionya kwamba mchakato huo unaweza kuhusisha Ukraine kutoa eneo fulani, matokeo ambayo Zelensky amekuwa akiyakataa mara kwa mara.

Mwandishi wa habari wa Australia aliyefukuzwa kazi kwa ujumbe kuhusu Gaza alipwa $150,000

h
Maelezo ya picha,Kufukuzwa kwa Antoinette Lattouf kulizua wimbi la hasira ya umma

Shirika la utangazaji la taifa la Australia limeagizwa kulipa A$150,000 (£73,435.50, $99,200) kama adhabu kwa kumfukuza kinyume cha haki mtangazaji kutokana na chapisho la mtandao wa kijamii kuhusu vita vya Gaza.

Shirika la Utangazaji la Australia (ABC) lilimwondoa mtangazaji wa redio Antoinette Lattouf hewani mnamo Desemba 2023 kwa sababu ya maoni yake ya kisiasa na baada ya ushawishi kutoka kwa vikundi vinavyounga mkono Israeli, Mahakama ya Shirikisho ilipata mapema mwaka huu.

Lattouf tayari ametunukiwa fidia ya A$70,000, lakini Jumatano Jaji Darryl Rangiah alisema kiasi “kikubwa” cha ziada kilihitajika ili kuhakikisha ABC inajifunza somo lake.

Mtangazaji huyo ameomba msamaha hadharani kwa Lattouf, akisema pia iliwafelisha wafanyikazi wake na watazamaji.

Kufukuzwa kwa Lattouf kulizua wimbi la hasira ya umma na kuzua taharuki katika shirika la ABC – na kuibua maswali juu ya uhuru wake na kuibua wasiwasi kuhusu jinsi inavyosaidia wafanyikazi, hasa wale ambao wana utamaduni tofauti.

“ABC ilidhalilisha umma wa Australia vibaya iliposalimisha haki za mfanyakazi wake … ili kutuliza kikundi cha watetezi,” Jaji Rangiah alisema Jumatano.

Macron kukutana na Masoud Pezeshkian kujadili mpango wa nyuklia wa Iran

g

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema atakutana leo na mwenzake wa Iran Masoud Pezeshkian kujadili mpango wa kinyuklia wa Iran miongoni mwa masuala mengine.

Akihutubia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unaofanyika New York, Bwana Macron ameonya kuwa vikwazo vikali vya Umoja wa Mataifa huenda vikarejeshwa kama Iran haitaruhusu shirika la kudhibiti matumizi ya silaha za kinyuklia kufanya kazi.

g
Maelezo ya picha,Rais wa Iran Masoud Pezeshkian

Viongozi wa Ulaya walikutana na waziri wa mambo ya kigeni hapo jana lakini hakukupigwa juhudi zozote.

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesisitiza nchi hiyo haitashinikizwa kuachana na mpango wake wa kinyuklia.

Iran ina mpaka Jumamosi hii kufikia makubaliano na mataifa yenye nguvu ya Ulaya la sivyo irejeshewe vikwazo vilivyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa vilivyoondolewa baada ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015.

Rais wa Somali aiambia BBC amenusurika majaribio kadhaa ya Al-shabab yaliyolenga kumuua

g

Rais wa Omalia Hassan Sheikh Mohamud amefichua kwamba sasa yeye ni shabaha kuu ya al-Shabaab, kikundi cha Kiislamu chenye mafungamano na Al-Qaeda.

Katika mahojiano marefu ya kipekee na BBC, alisema alikuwa amenusurika majaribio kadhaa ya mauaji na kikundi hicho.

“Kwa miaka miwili iliyopita, al-Shabaab wamenijaribu mara tano, kwa sababu wanaamini mabadiliko ambayo wanaweza kuzima vita dhidi yao ni kumuua rais. Miji mingi imekombolewa kutoka kwa al-Shabaab lakini bado inafanya kazi katika maeneo ya vijijini. Al-Shabaab ni dhaifu ikilinganishwa na maisha yao ya zamani.”

Somalia inakabiliwa na vitisho vya usalama kutoka kwa al-Shabaab na ISIS, licha ya uingiliaji kati wa kijeshi wa vikosi vya Umoja wa Afrika na Marekani.

Wachambuzi wanasema kuwa mafanikio ya hivi karibuni ya al-Shabaab katika Somalia ya kati na kusini yanaonyesha kwamba kundi hilo bado ni tishio kubwa.

Pia alithibitisha uwepo wa vikosi vya Jubaland nchini Kenya.

“Wamevuka kwenda Kenya, na wako huko Mandera. Hatujafurahishwa na hilo, na tumeshiriki wasiwasi wetu na serikali ya Kenya, na waliahidi kwamba watachukua hatua, na tutaenda pamoja na kufanyia kazi usalama wa eneo la mpaka.”

Wakati akizungumzia masuala ya kikanda rais aliapa kuendeleza kupelekwa kwa wanajeshi wa Misri nchini mwake, licha ya wasiwasi kwamba inaweza kuongeza mvutano na nchi jirani ya Ethiopia.

Alipuuzilia mbali ripoti za uwezekano wa makabiliano kati ya walinda amani wa Misri na Ethiopia katika ardhi ya Somalia. Somalia inajiandaa kuwapokea walinda amani wa Misri wakati wa kukaribisha vikosi vya Ethiopia.

Kuna wasiwasi kwamba nchi zote mbili zinaweza kupanua mpasuko wao juu ya Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance hadi Somalia. Alisisitiza kuwa nchi yake haitakuwa uwanja wa vita vya wakala.

Mwanaume apatikana na hatia ya kujaribu kumuua Trump Florida

g

Ryan Routh amepatikana na hatia ya kujaribu kumuua Rais Donald Trump kwenye uwanja wa gofu wa Florida Septemba mwaka jana.

Mahakama ilimpata Routh, 59, na hatia ya mashtaka yote, ikiwa ni pamoja na jaribio la mauaji ya mgombea mkuu wa urais na makosa kadhaa ya kutumia silaha.

Tukio hilo lilitokea tarehe 15 Septemba 2024 wakati Trump, ambaye wakati huo alikuwa mgombea urais, alikuwa akicheza gofu kwenye uwanja anaoumilik uliopo katikaufukwe wa West Palm Beach, takriban dakika 15 kutoka kwa makazi yake ya Mar-a-Lago.

Routh alijaribu kujidhuru baada ya hukumu kusomwa, kulingana na mshirika wa BBC wa Marekani, CBS News. Inasemekana alijaribu kujichoma kisu kwa kutumia kalamu kabla ya Wanajeshi wa Marekani kuingilia kati.

Katika chapisho la mtandao wa kijamii mara baada ya hukumu hiyo, Trump alishukuru vyombo vya sheria na shahidi ambaye alitoa taarifa zilizofanikisha kukamatwa kwa Routh.

Trump alisema kuhusu Routh: “Huyu alikuwa mtu muovu mwenye nia mbaya, na walimkamata. Wakati mkubwa sana kwa HAKI NCHINI AMERIKA!”.

Mwanasheria mkuu wa serikali Pamela Bondi alisema: “Jaribio hili la kumuua halikuwa tu shambulio kwa rais wetu, bali ni dharau kwa taifa letu.”

Idadi ya majeruhi wa shambulio la Israel Mjini Gaza yawalemea madaktari

g
Maelezo ya picha,Baadhi ya Wapalestina waliouawa wakati wa mashambulizi ya Israel katika mji wa Gaza wanazikwa katika uwanja wa hospitali ya al-Shifa.

Madaktari katika hospitali moja ya mwisho ya Jiji la Gaza wanasema wamelemewa na majeruhi kutokana na mashambulizi ya Israel na wanalazimika kufanya oparesheni katika mazingira machafu na hakuna dawa za ganzi.

Daktari mmoja wa Australia anayejitolea katika hospitali ya al-Shifa aliambia BBC kwamba kila siku kulikuwa na tukio la majeruhi wengi, huku mwingine akielezea jinsi mtoto mchanga alivyookolewa kutoka kwa mwili wa mwanamke mjamzito ambaye alikuwa amekatwa kichwa.

Vikosi vya Israel kwa sasa viko umbali wa mita 500 tu kutoka hospitali huku wakipanua mashambulizi yao ya ardhini ili kuliteka kikamilifu Jiji la Gaza, ambalo jeshi la Israel linaiita Hamas “ngome kuu”.

Walioshuhudia wanasema vifaru vinaingia katikati mwa jiji kutoka kusini na kaskazini-magharibi.

Mashambulio ya anga na mizinga ya Israel, mashambulio ya ndege zisizo na rubani na ulipuaji wa magari yanayoendeshwa kwa mbali yakiwa na vilipuzi yanaendelea kuwafukuza makumi ya maelfu ya Wapalestina kutoka makwao kila siku.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment