Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna mafunzo katika hayo maumivu…
There are lessons in your pain…
Nimegundua kuwa unapopitia mambo magumu kwenye maisha sio…
Kwa ajili ya kukuumiza tu ila ni kwa ajili ya kujifunza pia.
Usipojifunza katika maumivu unayopitia au uliyopitia leo uwe na uhakika yatajirudia tena kesho.
Unasikia kuumia kwa sababu kuna mtu alikuahidi kitu na ukaweka matumaini 100%…
Ukaacha kila kitu kingine kwa matumaini ya hiyo ahadi.
Ukaweka nguvu na hata pesa zako, ila mwisho wa siku hajafanya na haonyeshi KUJALI.
Unafundishwa kuwa mwanadamu ni kigeugeu…
Ni hatari kuweka tumaini kwake hata kama anaapa kuwa atafanya, umtumainie Mungu zaidi.
Unapopitia maumivu ya kusalitiwa na uliowaamini sana katika maisha yako…
Unapewa somo la KUCHAGUA nani wa KUMUAMINI na mambo yako.
Badala ya kusema watu wote hawafai, jifunze kuchagua na kutokuwa na haraka katika kuwaamini wengine.
Unapopitia maumivu ya KUKATALIWA kwenye maisha…
Unajifunza kutambua kuwa sio kila mtu ataiona thamani yako.
Unatambua kuna aina ya watu MUNGU amewaandaa wakupokee…
Na kuna wengine hata iweje HAWATAKUKUBALI bila kujali kiwango cha WEMA WAKO.
Badala ya kutumia nguvu nyingi kukubalika na kila mtu…
Unaamua KUJIKITA katika wale ambao kwa wakati huo wameandaliwa kwa ajili yako.
Unapokuwa HAUPATI unachotaka kwa Muda mrefu, kuna maumivu ya kujiona umepungukiwa sana.
Hili ni somo linatusaidia pale tutakapopata TUWAJALI wasionacho pia.
Badala ya kudhania WEMA na AKILI zetu zimetupa tulivyonavyo…
Unaanza kugundua kuwa ni NEEMA ya MUNGU ndio imetusaidia na TUSIWADHARAU watu walioletwa mbele yetu.
USIYACHUKIE MAUMIVU, USIWACHUKIE WALIOKUUMIZA, Jiulize “UMEJIFUNZA NINI?
Ukichelewa kupata somo, maumivu yataendelea ama yataacha na yatarudi tena.
Umeshawahi kupitia maumivu na ukajifunza kitu cha kukusaidia?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.