Uvumilivu hula Mbivu..

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna mambo kwenye maisha HAYATATOKEA haraka kama unavyotaka…

Kuna watu kwenye maisha hautafahamiana nao kwa haraka kama unavyotaka.

Kuna FURSA kwenye maisha hautazipata kwa haraka kama unavyotaka.

Mara nyingi kukiwa na hali ya KUCHELEWA kwenye tunachokitaka…

…huwa tunaamini inamaanisha TUMEACHWA, SIO KWELI.

Kuna wakati UPEO wa macho yetu unakuwa mdogo sana kuweza kuona kila KITU…

Na huwa tunatamani na kufanya bidii KUPATA FURSA…

Na KUJUANA na watu ambao baada ya muda mfupi wanaweza kugeuka kuwa SUMU kwetu.

Kwa sababu Mungu anatupenda na hataki tufikie huko…

Anahakikisha tunachokitaka hatukipati na tunayemtaka hatumpati kwa wakati huo:

Sio kwa sababu HATUJALI ila kwa sababu ANATUJALI sana na HATAKI TUANGAMIE.

Hii ndio maana, usilazimishe mahusiano na ukaribu na mtu ambapo moyoni kuna ukakasi.

Kwa upande mwingine kuna WATU ambao tunawaona wa kawaida sana na hawana msaada wa maana leo…

Lakini kwa sababu JICHO la MUNGU huwa linaona mbali anajua UMUHIMU wao kwa maisha yako ya KESHO….

…na ameamua kukukutanisha nao leo, USIWADHARAU.

Kuna fursa ambazo ukiziangalia na Kuzitathmini unaziona NDOGO na sio HADHI yako kwa leo…

Lakini Mungu amezileta ili azitumie kukukutanisha na WATU…

Au FURSA zingine zitakazobadilisha maisha yako – USIZIDHARAU!

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment