Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kitu kingine kikubwa sana ambacho kinaathiri sana mitazamo yetu (Attitude)…
….juu ya mambo tunayopitia ni maneno ambayo tunajiambia wenyewe kila siku.
Professor Charles Fernyhough kutoka chuo kikuu cha Durham nchini Uingereza aliwahi kufanya utafiti…
…na kungundua kuwa kwa dakika moja mtu hujisemesha maneno takribani 4,000.
Ambayo ni mara kumi zaidi ya maneno ambayo mtu anayaongea kwa mdomo kwa dakika.
Hataka kama hautaki, bado ndani yako kutakuwa na mazungumzo ambayo yanaendelea.
Swali ni kuwa, Je huwa unajisemesha maneno gani?
Watu wengi sana huwa wanajisemesha maneno yanayowasababisha…
…washindwe na wasifanikiwe katika maisha.
Kuna watu wakiamka tu, huwa wanaanza kujiongelesha ndani ndani kuwa
“Hawawezi…
Hawatafanikiwa…
Watafeli…
Wamefika mwisho n.k”…
Hii huwasababisha kuanza siku yao vibaya…
…na kutokuwa na matumaini kabisa ya kupata mafanikio ya maisha.
Kwa sababu mengi tunayoyasikia na kuyaona kila siku ni mambo hasi…
…basi kinachotokea ni kuwa mawazo ya ndani yetu huwa ni HASI tu!
Ili tujikinge na kuwaza hasi lazima ujifunze kujisemesha.
Anza siku yako kwa kujiambia.
“Mimi ni Mshindi”…
“Hata katika hili nitapita salama”…
“Naamini nitainuia tena” n.k…
Leo, kila unapohisi kuna sauti hasi ndani yako, fanya bidii kujisemesha kwa SAUTI mambo CHANYA…
Wewe unaanza kwa kujisemesha nini leo?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.