Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameshtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 80 anatuhumiwa kuhusika na uhalifu wa mauaji kadhaa ambayo yanadaiwa kutokea kama sehemu ya kile kinachoitwa vita vyake dhidi ya dawa za kulevya, ambapo maelfu ya wafanyabiashara wadogo wa dawa za kulevya, watumiaji na wengine waliuawa bila kufunguliwa mashtaka.
Waraka wa mashtaka ya ICC, ambao ulikuwa na marekebisho kadhaa, ulionyesha mashtaka hayo yalianzia Julai lakini uliwekwa wazi Jumatatu.
Naibu mwendesha mashtaka wa ICC, Mame Mandiaye Niang alisema kuwa Duterte alikuwa “mshiriki asiye wa moja kwa moja” katika mauaji hayo, ambayo mahakama inadai yalitekelezwa na watu wengine wakiwemo polisi.
Kesi ya kwanza iliyotolewa dhidi ya Bw Duterte inahusu madai yake ya kuhusika katika mauaji ya watu 19 katika Jiji la Davao kati ya 2013 na 2016 alipokuwa meya huko.
Mashtaka mengine mawili yanahusiana na wakati alipokuwa akihudumu kama rais wa Ufilipino, kati ya 2016 na 2022, na kuanzisha kile kinachojulikana kama vita dhidi ya dawa za kulevya.
Hesabu ya pili inahusiana na mauaji ya “walengwa wa thamani ya juu” 14 kote nchini, wakati ya tatu inahusiana na mauaji na jaribio la mauaji ya watu 45 katika shughuli za uondoaji kijiji.
Waendesha mashtaka walirejelea jinsi Bw Duterte na watuhumiwa wenzake “walishiriki mpango au makubaliano ya pamoja ya ‘kuwaondoa’ wahalifu wanaodaiwa nchini Ufilipino (ikiwa ni pamoja na wale waliodhaniwa au wanaodaiwa kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya, uuzaji au uzalishaji) kupitia uhalifu wa kikatili ikiwa ni pamoja na mauaji”.
Hajatoa pole kwa ukandamizaji wake wa kikatili wa kupambana na dawa za kulevya, ambao ulisababisha zaidi ya watu 6,000 kuuawa – ingawa wanaharakati wanaamini kuwa idadi halisi inaweza kufikia makumi ya maelfu.
Nchi tatu za Afrika Magharibi kujiondoa katika mahakama kuu ya Kimataifa ya uhalifu ICC

Burkina Faso, Mali na Niger zimetangaza uamuzi wao wa kujiondoa mara moja kuwa wanachama wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita na kibinadamu ICC,zikidai mahakama hiyo ni chombo cha kuendekeza ukoloni mambo leo na ubaguzi katika hukumu zake.
Mataifa hayo matatu ya ukanda wa Sahel katika taarifa ya pamoja iliyoidhinishwa na Jenerali Assimi Goita rais wa Mali imeshutumu ICC kwa kuwaandama bila kukoma viongozi fulani hasa wa kutoka mataifa masikini na kudhihirisha kushindwa kuwahukumu wanaofanya uhalifu mbaya zaidi ulimwenguni.
Uamuzi huo ndiyo wa hivi karibuni kutoka kwa mataifa hayo matatu ya magharibi mwa Afrika ynayoongozwa kijeshi ambayo pia mwaka huu yalijiondoa kutoka jumuiya ya maendeleo ya nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS na kuanzisha jumuiya ya mataifa ya Sahel AES.
ICC iliyoanzishwa mwaka 2002 ilitiwshwa jukumu la kushughulikia kesi za mauaji ya halaiki,uhalifu dhidi ya binadamu na vita na tangu wakati huo imepokea mashitaka thelathini na tatu.
Wakosoaji wa ICC wanasema mahakama hyiyo inawalenga viongozi wa Afrika lakini wanaoiunga mkono wanahoji mfumo dhaifu wa idara za mahakama katika mataifa ya Afrika zinalazimu asasi na watu binafsi kutafuta haki katika mahakama hiyo ya kimataifa.
Ufaransa yalitambua rasmi taifa la Palestina

Ufaransa imelitambua rasmi taifa la Palestina, na kuwa nchi ya hivi punde zaidi katika wimbi la nchi kuchukua hatua hiyo.
Akizungumza katika Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Emmanuel Macron alisema “wakati wa amani umefika” na kwamba “hakuna kinachohalalisha vita vinavyoendelea Gaza”.
Ufaransa na Saudi Arabia zinaandaa mkutano wa siku moja katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoangazia mipango ya suluhu la mataifa mawili katika mzozo huo. Mataifa ya G7 Ujerumani, Italia na Marekani hawakuhudhuria.
Ubelgiji, Luxembourg, Malta, Andorra na San Marino pia zinatarajiwa kulitambua taifa la Palestina, baada ya Uingereza, Canada, Australia na Ureno kutangaza kulitambua Jumapili.
Shinikizo la kimataifa linaongezeka kwa Israeli juu ya mgogoro wa kibinadamu unaoendelea huko Gaza na ujenzi wa makazi katika Ukingo wa Magharibi.
Israel imesema kutambuliwa kwake ni zawadi kwa Hamas kwa shambulio la kundi la wapiganaji la Palestina la tarehe 7 Oktoba 2023 kusini mwa Israel ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na 251 kuchukuliwa mateka.
Zaidi ya Wapalestina 65,000 wameuawa na Israel tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas. Vikosi vya Israel kwa sasa vinafanya mashambulizi ya ardhini yenye lengo la kuudhibiti mji wa Gaza, ambako watu milioni moja walikuwa wakiishi na njaa ilithibitishwa mwezi uliopita.
Kiongozi huyo wa Ufaransa aliuambia mkutano huo kuwa wakati umefika wa kusitisha vita na kuwakomboa mateka waliosalia wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas. Alionya dhidi ya “hatari ya vita visivyoisha” na kusema “haki lazima itashinda nguvu kila wakati”.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.