Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Haya ndiyo mambo 10 yanayokukwamisha kupata matokeo..
1.Kuwa na maudhui zenye mwonekano mbaya.
Mwonekano mzuri huvutia wateja. Unahitaji kuwa na picha safi, video bora na ukurasa (page) uliopangiliwa vizuri.
2. Kuuza bidhaa badala ya thamani
Wateja hununua thamani au suluhisho la tatizo lao, sio tu bidhaa. Jitahidi kuonesha thamani na faida za kile unachouza.
3. Kutumia sana maandishi bila video
Mitandao ya kijamii inapendelea kusambaza video zaidi kuliko maandishi. Wale wanaotumia video ndio hupata matokeo makubwa.
4. Kukosa mwendelezo
Mwendelezo hujenga jina na husaidia kuteka soko kwa urahisi. Bila mwendelezo ni vigumu watu kukuamini.
5 Kushindwa kufunga mauzo
Baada ya mteja kukutumia ujumbe, unahitaji hatua za kumshawishi alipe. Usianze na bei kabla ya kuonesha thamani na matokeo atakayopata.
6. Kushindwa kutengeneza content zenye ushawishi
Unahitaji content za kuelimisha, shuhuda za wateja, na maelezo ya bidhaa zako. Panga ratiba ya content ili uone matokeo makubwa.
7. Kushindwa kuuza kama mtaalamu
Watu hununua kwa wale wanaoonekana kuwa waaminifu na wataalamu. Jifunze kuelimisha jamii na wateja wako ili wakutumainie.
8. Kutokujua wateja wako vizuri
Wajasiriamali wengi huanza kuuza bila kuelewa ni nani hasa wateja wao, matatizo yao ni yapi, na wanapatikana wapi.
8. Kutokuwekeza kwenye matangazo (ads)
Kama hutumii matangazo ya kulipia ili kufikia watu wengi zaidi, ni rahisi kukwama kwa kutegemea organic reach pekee.
10. Kukata tamaa mapema
Biashara online inahitaji uvumilivu. Wengi hukata tamaa baada ya muda mfupi bila kuona matokeo, badala ya kujifunza na kuboresha mbinu.
Ni jambo gani ambalo bado linakusumbua kati ya haya..?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.