Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Uingereza kutangaza kulitambua taifa la Palestina siku ya Jumapili

Sir Keir Starmer anatarajiwa kutangaza kulitambua taifa la Palestina katika taarifa yake Jumapili mchana.
Hatua hiyo imekuja baada ya waziri mkuu kusema mwezi Julai kwamba Uingereza itabadilisha msimamo wake mwezi Septemba ikiwa Israel haitatimiza masharti ikiwa ni pamoja na kukubaliana kusitisha mapigano Gaza na kujitolea kwa makubaliano ya muda mrefu ya amani ambayo yatatoa suluhu la mataifa mawili.
Inawakilisha mabadiliko makubwa katika sera ya kigeni ya Uingereza baada ya serikali zilizofuata kusema kutambuliwa kunapaswa kuja kama sehemu ya mchakato wa amani na wakati wa athari kubwa.
Hatua hiyo imezua shutuma kali kutoka kwa serikali ya Israel, familia za mateka na baadhi ya wahafidhina.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hapo awali alisema hatua kama hiyo “inaunga mkono ugaidi”.
Hata hivyo, mawaziri wa Uingereza wanahoji kuwa kulikuwa na jukumu la kimaadili la kuchukua hatua ili kuweka hai matumaini ya mpango wa amani wa muda mrefu.
Vyanzo vya serikali vilisema hali ilikuwa mbaya zaidi katika wiki chache zilizopita. Walitoa picha zinazoonesha njaa na ghasia huko Gaza, ambayo waziri mkuu ameitaja kuwa “isiyovumilika”.
Operesheni ya hivi karibuni ya Israel katika mji wa Gaza, iliyoelezewa na afisa wa Umoja wa Mataifa kama “janga”, imewalazimu mamia kwa maelfu ya watu kukimbia.
Mapema wiki hii, tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ilihitimisha kuwa Israel ilifanya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina huko Gaza, ambayo Israel iliyashutumu kuwa ” potofu na ya uongo”.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.