Trump aongeza ada ya $100,000 kwa waomba viza wenye ujuzi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini agizo la rais ambalo litaongeza ada ya kila mwaka ya $100,000 (£74,000) kwa waombaji katika mpango wa visa wa H-1B kwa wafanyikazi wa kigeni wenye ujuzi.

Agizo la Trump linataja “matumizi mabaya” ya programu na litawazuia watu kuingia Marekani hadi malipo yatakapozingatiwa.

Wakosoaji kwa muda mrefu wamekuwa wakibishana kuwa H-1Bs inapunguza nguvu kazi ya Marekani, wakati wafuasi – ikiwa ni pamoja na bilionea Elon Musk – wanasema inaruhusu Marekani kuvutia vipaji vya juu kutoka duniani kote.

Katika utaratibu mwingine, Trump alianzisha “kadi ya dhahabu” mpya ili kuharakisha utoaji wa viza kwa wahamiaji badala ya ada ya kuanzia £1m.

Agizo la Trump linatarajiwa kuanza kutumika tarehe 21 Septemba.

Ingetumika tu kwa maombi mapya, lakini makampuni yangelazimika kulipa kiasi sawa kwa kila raia wakigeni kwa miaka sita, Waziri wa Biashara wa Marekani Howard Lutnick alisema.

Wanane wakamatwa Malawi kwa madai ya udanganyifu katika uchaguzi

Raia wa Malawi walipiga kura katika uchaguzi wa rais, wabunge na mitaa siku ya Jumanne
Maelezo ya picha,Raia wa Malawi walipiga kura katika uchaguzi wa rais, wabunge na mitaa siku ya Jumanne

Polisi nchini Malawi wamewakamata watu wanane kwa madai ya udanganyifu katika uchaguzi wakati nchi hiyo ikisubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumanne.

Inspekta Jenerali Merlyne Yolamu anasema washukiwa hao ambao walikuwa wakifanya kazi kama makarani wa uwekaji data wamekuwa wakijaribu kuvurga takwimu hizo.

Uchaguzi wa Malawi wa 2019 ulikumbwa na utata wakati mahakama ya juu zaidi ilipobatilisha ushindi wa Rais wa wakati huo Peter Mutharika, ikitaja kasoro zilizojitokeza wazi.

Kutokana na uamuzi huo, Tume ya uchaguzi ya Malawi imekuwa katika hali ya tahadhari kukabiliana na masuala yoyote yanayoweza kutokea.

Matokeo ya kura zilizohesabiwa rasmi kufikia sasa, zinaonyesha Mutharika ndiye anayeongoza kinyang’anyiro cha urais huku Rais wa sasaLazarus Chakwera akishika nafasi ya pili.

Matokeo zaidi kutoka katika wilaya 36 za Malawi yanatarajiwa kutolewa Jumamosi – mgombea anahitaji kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura, mshindi wa

Ureno yathibitisha kuwa italitambua taifa la Palestina

Maandamano yamefanyika nchini Ureno kushinikiza kusitishwa kwa mapigano huko Gaza
Maelezo ya picha,Maandamano yamefanyika nchini Ureno kushinikiza kusitishwa kwa mapigano huko Gaza

Ureno inasema italitambua taifa la Palestina siku ya Jumapili, na kulifanya taifa la hivi punde zaidi la Magharibi linalojiandaa kubadili sera kwani vita katika Ukanda wa Gaza havionyeshi dalili ya kusitishwa.

Wizara ya mambo ya nje imetoa tangazo hilo kabla ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) utakaofanyika wiki ijayo mjini New York.

Ufaransa, Uingereza, Canada na Australia zinajiandaa kutoa matangazo sawa na hilo.

Israel imelaani hatua hiyo, huku Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akisema “inatukuza ugaidi” kufuatia shambulio la Hamas la tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya Israel.

Marekani – mshirika mkuu wa Israel – inaunga mkono hoja ya Netanyahu.

Akizungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer wiki hii katika ziara ya kitaifa nchini humo, Rais wa Marekani Donald Trump, alisema hakubaliani na na hatua ya kulitambua taifa la Palestina.

Takriban robo tatu ya wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa tayari wanalitambua taifa la Palestina, ambalo mwaka 2012 lilipewa hadhi ya kuwa nchi isiyokuwa mwanachama.

Viongozi wa dunia wakijiandaa kukusanyika katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne ijayo, vifaru vya wanajeshi wa Israel vinaendelea kuingia katika mji wa Gaza kama sehemu ya mashambulizi ya ardhini, ambayo yamewalazimu maelfu ya watu kukimbia mji huo.

Jeshi la Israel lilianzisha operesheni huko Gaza kujibu mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas kusini mwa Israel mwaka 2023, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 251 watekwa nyara.

Takriban Wapalestina 65,141 wameuawa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment