Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watoto wa Kipalestina wakijiandaa kutoroka kaskazini mwa mji wa Gaza baada ya amri ya Israel ya kuwahamisha
Jeshi la Israel limeonya Ijumaa kwamba litatumia “nguvu zisizokuwa na kifani” katika Jiji la Gaza, na kutangaza kufungwa kwa Mtaa wa Salah al-Din kwa wakazi, walioonywa kuuhama mji huo na kuelekea kusini kupitia mtaa wa Rashid Coastal.
Jeshi lilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari, “Kwa wakaazi wa Mji wa Gaza, hadi kufikia sasa, Barabara ya Salah al-Din imefungwa kwa ajili ya kusafiri kuelekea kusini. IDF itaendelea kufanya kazi kwa nguvu isiyo na kifani dhidi ya Hamas na mashirika mengine ya kigaidi. Kufikia wakati huu, kusafiri kuelekea kusini kunaruhusiwa tu kupitia mtaa wa Rashid kwa usalama wako.”
Mapema Ijumaa, msemaji wa jeshi la Israel Avichay Adraee alitoa wito kwa wakazi wa mji wa Gaza kuchukua fursa ya kile alichokitaja kuwa “njia ya muda ya kusafiri” katika mtaa wa Salah al-Din, akisisitiza kuwa mtaa huo utakuwa wazi kwa harakati za umma hadi saa 12:00 jioni. wakati wa eneo.
Katika ujumbe wake kwenye tovuti yake ya X, Adraee aliishutumu Hamas kwa kujaribu “kuwatisha” wakazi na kuwazuia kuondoka jijini, akidai kuwa vuguvugu hilo linataka kuwatumia kama “ngao za binadamu”
Afisa wa Taliban apuuza matumaini ya Trump ya ‘kurudisha’ kambi ya anga ya Afghanistan

Afisa wa Taliban amepinga wazo kwamba Marekani inaweza kuchukua tena kambi muhimu ya anga nchini Afghanistan baada ya Rais Donald Trump kuwaambia waandishi wa habari kuwa anataka irejeshwe.
Zakir Jalal, ambaye anafanya kazi katika wizara ya mambo ya nje ya Taliban, amesema wazo la Marekani kudumisha uwepo wowote wa kijeshi nchini Afghanistan “imekataliwa” kabisa wakati wa mazungumzo kati ya pande hizo mbili kabla ya Taliban kurejea madarakani.
Hii ni baada ya rais wa Marekani kudokeza kuchukua tena kambi ya anga ya Bagram – kitovu cha vikosi vya Nato nchini Afghanistan kwa miongo miwili – huenda ikawezekana “kwa sababu wanahitaji vitu kutoka kwetu”.
Kambi hiyo ilikabidhiwa kwa jeshi la Afghanistan muda mfupi kabla ya Taliban kuchukua udhibiti wa Afghanistan.
Trump alisema katika mkutano na waandishi wa habari nchini Uingereza siku ya Alhamisi kwamba Marekani “iliwapa bure”.
Kuondolewa kabisa kwa wanajeshi wa Marekani ilikuwa sehemu ya makubaliano yaliyotiwa saini wakati wa utawala wa kwanza wa Trump mnamo 2020, na kukamilika chini ya Joe Biden mnamo 2021.
Lakini Trump alisema mnamo Machi kwamba anapanga kuweka kituo cha anga cha Bagram “si kwa sababu ya Afghanistan lakini kwa sababu ya Uchina.”
Shirika la ujasusi la Uingereza MI6 lazindua tovuti ya siri ili kuvutia wapelelezi nchini Urusi

MI6 inazindua tovuti yake maalum kwenye wavuti siri kwa matumaini ya kuwavutia wapelelezi wapya mtandaoni, hasusan kutoka Urusi.
Jukwaa hilo salama la kutuma ujumbe Silent Courier linalenga kuimarisha usalama wa taifa kwa kulirahisisha shirika la ujasusi kuajiri, Wizara ya mambo ya nje ilisema.
Idadi ya mawakala inayowezekana nchini Urusi na ulimwenguni kote watalengwa na Uingereza, wizara hiyo imeongeza.
Mkuu wa MI6 anayemaliza muda wake Sir Richard Moore Siku ya Ijumaa alitoa wito kwa majasusi watarajiwa duniani kote kufikia mtandao wa siri bila kujulikana kwa kufuata maagizo kwenye video ya MI6 ya YouTube.
Katika hotuba yake ya mwisho ya hadhara kama Mkuu wa MI6, Sir Richard alizindua harakati ya kuajiri watu ulimwenguni kote ikilenga majasusi wanaowezekana nchini Urusi, Uchina, Iran, Korea Kaskazini na kwingineko.
Katika hotuba hiyo hiyo aliyoitoa Istanbul siku ya Ijumaa asubuhi, alionyesha ukosoaji mkali dhidi ya Rais Putin, akisema “hakuna ushahidi” rais wa Urusi ana nia yoyote katika mazungumzo ya amani, “muda mfupi wa kujisalimisha wa Ukraine”.
“Anatudanganya”.
Aliongeza kuwa Putin hawezi kufanikiwa nchini Ukraine na akasema Putin “ameuma zaidi ya anavyoweza kutafuna.”
Mkuu huyo wa MI6 pia aliishutumu China kwa kuunga mkono juhudi za vita vya Urusi kidiplomasia na kwa kutumia bidhaa mbili kama vile “kemikali ambazo huishia kwenye makombora na vifaa vya kielektroniki ambavyo huishia kwenye makombora yao”.
Trump: Sikutaka meya wa London ahudhurie karamu ya kifalme

Rais wa Marekani Donald Trump amesema “hakutaka” Meya wa London Sadiq Khan kuhudhuria karamu ya serikali ya mfalme wa Uingereza katika kasri ya Windsor.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kurejea Marekani kwa ndege ya Air Force One, Bw Trump alimtaja Sadiq Khan kama “mmoja wa mameya wabaya zaidi duniani” na akasema alitaka kuhudhuria hafla hiyo lakini “nilimwomba asiwepo.”
BBC imefahamu kuwa Meya wa London hakutaka mualiko wala kutarajia kuhudhuria karamu hiyo.
Chanzo kilicho karibu na Bw Khan kilisema sera za Trump ni “uoga na mgawanyiko”.
Vita vya hivi punde vya maneno vimeongeza uhasama wa muda mrefu kati ya wawili hao huku Bw Trump akimuita meya wa London “mtu aliyeshindwa kabisa”
Mwaka wa 2019 na Sadiq Khan akimshutumu Trump kwa sera za mrengo mkali wa kulia.
Trump kwa mara nyingine aliukosoa utendakazi wa Meya wa London kwa utawala wa jiji hilo.
Rais wa Marekani alisema: “Nadhani meya wa London, Sadiq Khan, ni mmoja wa meya wabaya zaidi duniani. Nadhani amefanya kazi mbaya sana, uhalifu huko London unaongezeka.”
“Nilimtaka asiwepo. Nijuavyo, alitaka kuwa, lakini sikutaka hivyo.”

Ugomvi wa muda mrefu wa wawili hao ulianza 2015, wakati mwanasiasa huyo wa chama cha Labour alilaani pendekezo la Trump la kuwapiga marufuku Waislamu kusafiri kwenda Marekani. Mwaka mmoja baadaye, Bw Trump alimpinga meya huyo kwa mtihani wa IQ.
Rais wa Marekani pia alikosoa jinsi meya wa London alivyoshughulikia shambulio la kigaidi la London Bridge 2017.
Ziara ya kwanza rasmi ya Bw Trump nchini Uingereza mwaka wa 2019 ilikabiliwa na maandamano makubwa kuhusu sera zake kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, uhamiaji na haki za wanawake, wakati Sadiq Khan aliporuhusu puto maarufu ya “Baby Trump” kuruka kwenye uwanja wa Bunge.
Wanandoa wa Uingereza waliokuwa wakishikiliwa kwa miezi kadhaa na Taliban walioachiliwa kutoka gerezani

Wanandoa wa Uingereza waliokuwa wakizuiliwa kwa takriban miezi minane na kundi la Taliban nchini Afghanistan wameachiliwa huru, afisa anayefahamu tukio hilo amesema.
Peter Reynolds, 80, na mkewe Barbie, 76, ambao wameishi nchini kwa karibu miongo miwili, walishikiliwa baada ya kusimamishwa walipokuwa wakisafiri kuelekea nyumbani tarehe 1 Februari.
Wanandoa hao waliachiliwa kupitia upatanishi wa Qatar, baada ya kuhamishwa kutoka gereza kuu la Kabul hadi gereza kubwa wakati wa awamu ya mwisho ya mazungumzo, afisa huyo alisema.
Afisa wa Qatar alisema wanandoa hao watasafiri kwa ndege hadi Qatar kwa uchunguzi wa afya kabla ya kusafiri kwenda Uingereza, licha ya kuwa na nyumba ya muda mrefu katika mkoa wa Bamiyan wa Afghanistan.
Kuachiliwa kwao kunafuata miezi kadhaa ya ushawishi wa umma na familia zao ili waachiliwe.
Siku sita tu zilizopita, mwanamke wa Kimarekani ambaye alizuiliwa nao na kuachiliwa aliiambia BBC kwamba “wanakufa” gerezani na kwamba “muda unasonga”.
Faye Hall, ambaye aliachiliwa kwa miezi miwili , alisisitiza kwamba afya ya wenzi hao wazee ilikuwa imezorota haraka walipokuwa gerezani.
Taliban yapiga marufuku vitabu vilivyoandikwa na wanawake katika vyuo vikuu Afghanistan

Serikali ya Taliban imeondoa vitabu vilivyoandikwa na wanawake katika mfumo wa kufundisha wa vyuo vikuu nchini Afghanistan kama sehemu ya marufuku mpya ambayo pia imeharamisha ufundishaji wa haki za binadamu na unyanyasaji wa kijinsia.
Baadhi ya vitabu 140 vya wanawake – ikiwa ni pamoja na “Safety in the Chemical Laboratory” – vilikuwa miongoni mwa vitabu 680 vilivyopatikana kuwa “visivyo sahihi” kutokana na “sera za kupinga Sharia na Taliban”.
Vyuo vikuu vilielezwa kuwa haviruhusiwi tena kufundisha masomo 18, huku afisa wa Taliban akisema “vinakinzana na kanuni za Sharia na sera ya mfumo”.
Amri hiyo ni ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa vikwazo ambavyo Taliban wameviweka tangu warudi madarakani miaka minne iliyopita.
Familia Kenya yashtuka na taarifa za mwanariadha aliyekamatwa Ukraine

Familia na marafiki wa mwanariadha wa Kenya wanasema wameshtuka baada ya kujua kuwa mtoto wao amekamatwa nchini Ukraine.
Vikosi vya Ukraine vilitoa video ya Evans Kibet, ambao wanasema alikuwa anapigana kwa niaba ya vikosi vya Urusi.
Katika rekodi ya video, mwanariadha anadai kwamba alidanganywa kujiunga na jeshi la Urusi wakati ametembelea nchi hiyo kama mtalii.
Evans Kibet anasema safari yake ya St. Petersburg iliandaliwa na wakala wa michezo na kufadhiliwa na serikali ya Urusi.
Aliiambia vikosi vya Ukraine kwamba mwishoni mwa safari yake, pasipoti yake na simu zilichukuliwa, na alilazimishwa kusaini hati zilizoandikwa kwa Kirusi, bila kujua alikuwa akisajiliwa kama mwanajeshi.
Baada ya wiki ya mafunzo ya kimsingi na kukabidhiwa bunduki, Kibet anasema alikataa kupigana.
Akatoroka na kujificha msituni kwa siku mbili, kabla ya kujisalimisha kwa wanajeshi wa Ukraine.
Katika video iliyotolewa na Ukraine anasihi asirudishwe Urusi akihofia maisha yake.
Serikali ya Urusi bado haijasema lolote kuhusiana na tukio hilo.
Waliofurushwa Marekani waishtaki Ghana kwa kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria

Watu 11 waliozuiliwa nchini Ghana baada ya kufukuzwa kutoka Marekani wameishtaki serikali ya taifa hilo la Afrika Magharibi, wakili wao ameiambia BBC.
Oliver-Barker Vormawor alisema waliofukuzwa hawakukiuka sheria yoyote ya Ghana, na kuzuiliwa kwao katika kambi ya kijeshi ni kinyume cha sheria.
Alitaka serikali iwafikishe watu hao mahakamani, na kusema kwa nini wanashikiliwa kinyume na matakwa yao, wakili huyo aliongeza.
Serikali bado haijatoa maoni yoyote kuhusu kesi hiyo, lakini hapo awali ilisema inapanga kuwapokea watu wengine 40 waliofukuzwa nchini Marekani.
Wabunge wa upinzani wanadai kusitishwa mara moja kwa mpango wa kuwapokea kuliofukuzwa hadi bunge litakapoidhinisha suala hilo, wakisema hatua hii inahitajika chini ya sheria za Ghana.
Uingereza yazindua tovuti maalum kuvutia majasusi wa Urusi

Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 limezindua tovuti maalum kwa matumaini ya kuvutia majasusi wapya mtandaoni, haswa kutoka Urusi.
Jukwaa salama la kutuma ujumbe Silent Courier linalenga kuimarisha usalama wa taifa na kurahisishia shirika la ujasusi kuajiri, Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilisema.
Mawakala nchini Urusi na ulimwenguni kote watalengwa na Uingereza, tovuti hiyo inaongeza.
Tangazo hilo linatarajiwa kuthibitishwa katika hotuba mjini Istanbul na mkuu wa shirika la MI6 anayeondoka Sir Richard Moore siku ya Ijumaa asubuhi.
Kabla ya tangazo la Ijumaa kuhusu tovuti hiyo mpya, Waziri wa Mambo ya Nje Yvette Cooper alisema: “Usalama wa kitaifa ni jukumu la kwanza la serikali yoyote na msingi wa Mpango wa Mabadiliko wa Waziri Mkuu.
“Dunia inapobadilika, na vitisho vinavyotukabili vinapoongezeka, lazima tuhakikishe kwamba Uingereza daima iko hatua moja mbele ya maadui zetu.
“Mashirika yetu ya kijasusi ya kiwango cha juu duniani yanakabiliwa na changamoto hii, yakijitahidi kwa kila namna kuhakikisha Usalama wa Waingereza.
“Sasa tunaimarisha juhudi zao kwa teknolojia ya hali ya juu ili MI6 iweze kuajiri majasusi wapya wa Uingereza – nchini Urusi na duniani kote.”
Vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwa Iran vitarudishwa, asema Rais Macron

Mataifa yenye nguvu ya Ulaya huenda yakaiwekea tena Iran vikwazo vya kimataifa ifikapo mwisho wa mwezi baada ya duru ya hivi karibuni ya mazungumzo na Iran kuzingatiwa kutochukuliwa kwa uzito unaostahili, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema siku ya Alhamisi.
Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, zinazojulikana kama E3, zilizindua mchakato wa siku 30 mwishoni mwa Agosti kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Waliweka masharti kwa Iran kuyatimiza mnamo mwezi wa Septemba.
Pendekezo la E3 la kuahirisha mazungumzo hayo kwa hadi miezi sita ili kuwezesha kuwa ya kina ni masharti kwa Iran kuruhusu ufikiaji wa wakaguzi wa nyuklia wa UN – ambao pia watajaribu kuangalia kiasi cha hifadhi ya Iran ya madini ya uranium yaliorutubishwa – na kushiriki katika mazungumzo na Marekani.
Alipoulizwa katika mahojiano kwenye Idhaa ya Channel 12 ya Israel ikiwa hatua hiyo ilikuwa imekubaliwa, Macron alisema:
“Ndiyo. Nafikiri hivyo kwa sababu taarifa za hivi punde kutoka kwa Wairani hazina uzito unaostahili.”
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi alisema baadaye siku ya Alhamisi kwamba aliwasilisha “mpango wa busara na unaoweza kutekelezeka kwa washirika wa E3/EU ili kuepusha mgogoro usio wa lazima na unaoweza kuepukika katika siku zijazo.”
Mawaziri wa mambo ya nje wa E3, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya na mwenzao wa Iran walipigiana simu siku ya Jumatano ambapo wanadiplomasia wa pande zote mbili walisema hakukuwa na maendeleo makubwa ingawa bado kuna fursa ya kufikia makubaliano kabla ya muda uliowekwa kufikia ukomo wake.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15 litapiga kura siku ya Ijumaa kuhusu azimio litakaloondoa kabisa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran – hatua ambayo inatakiwa kuchukuliwa baada ya E3 kuanzisha mchakato huo.
Azimio hilo huenda likashindwa kupata kiwango cha chini cha kura tisa zinazohitajika kupitisha, wanasema wanadiplomasia, na kama litapishwa huenda likapigiwa kura ya turufu na Marekani, Uingereza.
Trump ageuza njia na kulazimika kubadilisha helikopta akielekea Stansted

Helikopta iliyokuwa imembeba Rais wa Marekani Donald Trump ililazimika kuelekezwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Luton alipomaliza ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza.
Waziri wa Vyombo vya Habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt alisema “kutokana na tatizo dogo”, ndege hiyo ilitua kwenye “uwanja wa ndege wa ndani” kabla ya kufika Stansted karibu dakika 20 nyuma ya ratiba.
Alisema uamuzi huo ulichukuliwa “kutokana na tahadhari nyingi” na kuongeza kuwa rais na mke wake “walipanda salama helikopta nyingine”.
Huduma za dharura zilionekana kwenye lami huko Luton kufuatia kutua kwa ndege hiyo.
Picha tofauti zinaonyesha helikopta zote mbili za Trump, nje kidogo ya barabara ya Luton.
Ndege iliyombeba rais inajulikana kwa jina la Marine One.
Helikopta hizo zimewekewa mifumo ya ulinzi wa makombora na kuziba rada pamoja na vifaa vya elektroniki vilivyoundwa kustahimili mapigo ya sumakuumeme ya mlipuko wa nyuklia.
Marekani yapiga kura ya 6 ya turufu kwa Umoja wa Mataifa kuhusu vita vya Gaza

Marekani imepiga kura ya turufu siku ya Alhamisi katika mswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lingetaka usitishaji vita mara moja, usio na masharti na wa kudumu huko Gaza na kwamba Israel iondoe vikwazo vyote vya kupeleka misaada kwa wapalestina.
Mswada huo uliyoandaliwa na wajumbe 10 waliochaguliwa wa baraza la wanachama 15, pia ungetaka kuachiliwa mara moja, kwa heshima na bila masharti mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas na makundi mengine.
Ulipata kura 14 za ndio. Ilikuwa ni mara ya sita kwa Marekani kupiga kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu vita vya takriban miaka miwili kati ya Israel na Hamas.
“Njaa imethibitishwa huko Gaza – haijakadiriwa, haijatangazwa, alithibitishwa,” Balozi wa Denmark wa Umoja wa Mataifa Christina Markus Lassen akiambia baraza kabla ya kupiga kura.
“Wakati huo huo, Israel imepanua operesheni yake ya kijeshi katika Mji wa Gaza, na hivyo kuzidisha mateso ya raia. Matokeo yake, ni hali hii ya janga, kushindwa kwa binadamu ambako kumetulazimisha kuchukua hatua leo,” alisema.
Mji wa Gaza na maeneo yanayozunguka yanakabiliwa rasmi na njaa, na huenda ikaenea, wafuatiliaji wa njaa duniani walibainisha mwezi uliopita.
‘Zaidi ya 30 wamekufa kwa Ebola nchini Congo’, – Shirika la Afya Duniani

Shirika la Afya Duniani siku ya Alhamisi lilisema maambukizi 48 ya Ebola yamethibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na watu 31 wamekufa.
“Imepita wiki mbili tangu serikali ya DRC itangaze mlipuko wa Ebola …Hadi sasa, maambukizi 48 yamethibitishwa…, na watu 31 wamekufa,” mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari kupitia video kutoka makao makuu ya WHO huko Geneva.
Mlipuko huo, wa kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka mitatu, ulitangazwa mapema Septemba.
Shirika la Afya Duniani Jumapili lilisema limeanza kutoa chanjo kwa wafanyikazi wa afya walio mstari wa mbele na walio wasiliana na watu walioambukizwa virusi vya Ebola katika Mkoa wa Kasai nchini Congo, ambapo mlipuko umetangazwa.
WHO imesema dozi 400 za awali za chanjo ya Ervebo Ebola kutoka akiba ya dozi 2,000 nchini humo zimefikishwa Bulape, kitovu cha mlipuko huo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.