ZINGATIA MAMBO HAYA 10 UNAPOKWENDA KWENYE INTERVIEW YA KAZI.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watu wengi sana wanakosa kazi sio kwamba hawana vigezo ila kuna mambo ya msingi hawakuzingatia kabla ya kwenda interview. Fahamu haya..

..

1. Tafuta Taarifa za Taasisi Kabla Ya Kwenda

Jua historia, huduma/bidhaa na malengo ya taasisi hiyo kabla ya usaili. Hii itaonyesha umekuwa makini na una nia ya dhati kutaka kazi.

..

2. Vaa Kwa Heshima

Mavazi yako yawe ya kitaalamu na safi. Muonekano wako ni sehemu ya alama ya kwanza unayotoa. Wengi wamekosa kazi kwa kuvaa vibaya katika usaili

..

3. Jali Muda

Fika mapema angalau dakika 15 kabla ya muda wa interview. Hii inaonyesha heshima na utayari. Pia itakusaidia kuweza kujiandaa na kuvuta pumzi na kufahamu hali halisi na utafanya vizuri.

4. Usitumie Simu

Zima au weka simu kimya. Usaili ni muda wa kuonyesha umakini wako. Simu ni kikwazo cha wengi kupata kazi, utakuta wengi wanachart muda wa usaili hii ni hatari sana kwako.

5. Usitaje Kiwango cha Mshahara Mwanzoni

Weka msisitizo kwenye nafasi na fursa ya kutoa mchango wako, si pesa pekee. Sikiliza maelekezo ya ofisi utaratibu wao, ukitaja mshahara mwanzo itaonesha upo kimaslai na sio kazi.

6. Onyesha Ujasiri na Heshima

Salimia kwa heshima, kaa vizuri, weka macho kwa mhoji. Lugha yako iwe thabiti na yenye adabu.

7. Toa Thamani.

Eleza wazi ni kwa namna gani utaongeza thamani kwenye taasisi hiyo kwa ujuzi na uzoefu wako, waajiri wengi huzingatia thamani ambayo utaiongeza Kwenye taasisi.

8. Sikiliza Vizuri Maswali

Usikimbilie kujibu. Sikiliza kwa makini kisha jibu kwa utulivu na usahihi. Ukifanya tofauti unaweza kukosa kazi.

9. Jiandae na Maswali ya Kawaida Na Fanya Mazoezi Kabla.

Jiandae kueleza juu ya wewe ni nani, kwa nini unataka kazi hiyo, na kwa nini wao wakuchague wewe.Ukipata muda jiandae kisaikolojia kuwa utafanya vizuri sana.

10. Shukuru Mwishoni

Shukuru paneli ya wasaili kwa muda wao na nafasi ya kuhojiwa. Inaacha taswira ya heshima na unyenyekevu.

Kwa uzoefu wako wewe ni jambo gani lingine ni muhimu kuzingatia unapoenda kwenye chumba cha interview.?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment