Usijilinganishe na Mtu Yeyote.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwaka 1954 mwanasaikolojia maarufu Leon Festinger alikuja na fikra inayoitwa “Social Comparison”…

Hii ni ile tabia ya mwanadamu kujilinganisha na wengine kama njia ya kujitathmini.

Mtu anapofanya kwa njia nzuri anapojipojilinganisha na watu waliomzidi (Upward Comparison)…

…inaweza kukupa hamasa ya kufanya zaidi.

Na anapojilinganisha na walioko chini yake (Downward Comparison)…

…inakuridhisha kuwa umepiga hatua kuliko wao.

Hata hivyo kuna madhara Makubwa sana kisaikolojia ya…

…kujilinganisha na wengine katika namna inayoleta Hisia hasi (Negative Comparison).

Hii ni kwa sababu kuna tofauti:

Wewe unaangalia CHAKO KILICHOJIFICHA na unajilinganisha na WANACHOKUONYESHA

(Your Behind the Scene Vs Their Chosen Highlights).

Njia nzuri ni kuamua kuweka MALENGO YAKO na kufanya bidii KUYATIMIZA.

Amua kuwa bora kuliko ULIVYOKUWA JANA.

Amua kukamilisha ndoto yako badala ya kutaka KUSHINDANA na wengine.

USISAHAU KUWA KILA MTU YUKO KATIKA WAKATI TOFAUTI WA MAISHA YAKE.

Focus on Your Goals!

USIUMIE kwa sababu wengine wamepiga hatua mbali sana kuliko wewe.

Umia kwa sababu UNASHINDWA kuchukua HATUA kila siku kukamilisha MALENGO YAKO.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment