Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kama wewe ni mfanyakazi na unataka kuanzisha biashara, zingatia makosa haya ya kawaida ambayo wengi hufanya ili uyepuke:
..
1. KUWEKA NDUGU NA KUAMINI HAWATAWAIBIA
Unapomuweka ndugu katika biashara yako, msimamie kama vile humjui.Ndugu pia ana mahitaji yake na anaweza kukutendea kama mfanyakazi mwingine yeyote.
Mara nyingi ndugu huamini umefungua biashara kwa ajili yake, na akiona una kazi na kipato kingine ataona huna hasara.
Msisimamie kwa hisia, msimamie kwa utaratibu wa kazi.
…
2. KUWEKA BIASHARA MBALI NA KAZI AU NYUMBANI
Ukiweka biashara sehemu ya mbali, itakua ngumu kufuatilia.
Weka sehemu karibu na nyumbani au kazini kwako, ili uweze kufika hata mara moja kwa wiki. Hii inasaidia kuisimamia na pia humfanya muuzaji awe mwangalifu kujua unaweza kufika ghafla.
…
3. KUANZA KULA BIASHARA KABLA HAIJAANZA KUJILIPA
Biashara mpya inahitaji muda kukua. Unaweza kuona mauzo makubwa lakini faida ni ndogo.
Usianze kujilipa mapema, acha biashara ikue kwanza.
…
4. KUFUNGUA BIASHARA NGUMU KUSIMAMIA
Chagua biashara ambayo unaweza kufuatilia kwa urahisi.
Epuka biashara inayokulazimisha safari ngumu au tegemeo kubwa la mtu mwingine.
Mfano: Biashara ya simu bila uwezo wa kwenda Dar kununua mzigo itakutesa.
…
5. KUSIKILIZA STORI ZA MTAANI
Usifungue biashara kwa sababu tu umesikia “inaingiza sana.”Wengi huanza bila utafiti, wakitarajia faida kubwa haraka.
Fanya utafiti wako, usitegemee maneno ya watu.
…
6. KUANZA NA MITAJI MIKUBWA AU MKOPO
Usitumie mtaji mkubwa mara moja, hasa ikiwa ni mkopo.
Ni busara kuanza kidogo, kujifunza sokoni, kisha kukuza hatua kwa hatua.
Mtaji ukigawanywa na kutumika kwa utaratibu hukulinda usipate hasara kubwa.
…
7. KUTOJIFUNZA ELIMU YA BIASHARA
Wengi wanaanza bila kusoma vitabu, kuhudhuria semina, au kupata ushauri wa kitaalamu.
Elimu inakusaidia kuandaa bajeti, kuendesha biashara na kuepuka hasara zisizo za lazima.
Jifunze kwanza kabla ya kuwekeza.
..
8. KUKOSA MFUMO WA KUMBUKUMBU
Biashara nyingi za wafanyakazi hufa kwa sababu hakuna mahesabu sahihi.
Bila kumbukumbu, hujui hasara wala faida.
Tumia daftari, app, au mfumo wa akiba ili kila senti ijulikane. Hasa tumia app kama Kuza Business na thl itakusaidia sana kuendesha na kuweka kumbukumbu vizuri.
…
9. KUAMINI BIASHARA ITAJIENDESHA PEKEE YAKE
Wengi hufikiria baada ya kuajiri mtu basi kazi imeisha.
Biashara bila usimamizi wako wa karibu mara kwa mara hufa.
Weka muda, hata kidogo, kufuatilia na kutathmini mwenendo wake.
…
10. KUKOSA SUBIRA NA KUFUNGA MAPEMA
Baadhi ya biashara zinahitaji muda kuota mizizi.Wafanyakazi wengi hukata tamaa haraka baada ya miezi michache bila faida.
Kuwa mvumilivu, rekebisha makosa badala ya kufunga mapema.
Ukiepuka makosa haya, biashara yako itakuwa na nafasi kubwa ya kukua na kukuletea uhuru wa kifedha hata kama bado unaendelea na kazi yako.
..
11. KUACHA KAZI MARA MOJA NA KUANZA BIASHARA.
.
Wengi wameangukia pua kwenye biashara kwani, biashara inapoanza huwa haizalishi faida, hivyo wengi hujikuta kutumia pesa ya mtaji na biashara kufa. Kama wewe ni mwajiriwa usifanye haraka kuacha kazi wakati unafanya biashara, iache iote miziz kwanza.
…
12.KUTOKUTOFAUTISHA KATI YA MISHAHARA NA BIASHARA
Wengi wanachanganya fedha ya mshahara na fedha ya biashara.
Wakipata mshahara, wanaongeza kwenye mauzo kana kwamba ni kitu kimoja, au wakihitaji hela haraka wanachukua kutoka kwenye biashara bila kurejesha.
Sheria ni kuwa mshahara ni mshahara, biashara ni biashara. Usichanganye.
Wewe unapata changamoto gani kati ya haya
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.