Baraza la usalama la UN kupiga kura kuidhinisha usitishwaji wa vita

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura kuidhinisha usitishwaji wa vita na kuruhusu misaada kuingia Gaza, licha ya kura turufu ya Marekani ambayo haiungi mkono hatua hiyo.

Wakimbizi wa Palestina wakiondoka katika Mji wa Gaza baada ya Israel kuwataka kufanya hivyo kutokana na oparesheni zake za ardhini.
Wakimbizi wa Palestina wakiondoka katika Mji wa Gaza baada ya Israel kuwataka kufanya hivyo kutokana na oparesheni zake za ardhini. AP – Abdel Kareem Hana

Wanachama 10 wasiokuwa wa kudumu wa baraza hilo walianzisha mchakato wa  kusitishwa kwa vita eneo la Gaza mwishoni mwa mwezi uliopita, baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwepo kwa baa la njaa eneo hilo kutokana na vita vya miaka miwili.

Rasmu ya mapendekezo hayo inajumuisha kuondoa vikwazo vya kutoa misaada na kusitishwa kwa vita mara moja, ila vyanzo vya habari vinasema kwamba mataifa ya UfaransaUingereza na Urusi, yameonyesha wasiwasi wao kuhusu, kiwango cha misaada kinachoelekezwa Gaza na Umoja wa Mataifa, kiwango ambacho Marekani imekuwa ikipinga na kutetea mshirika wake Israeli.

Le Conseil de sécurité de l'ONU réunit au siège des Nations unies à New York.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa © Eduardo Munoz / REUTERS

Wacahama wengine 14 wa baraza hilo la Umoja wa Mataifa wamekuwa wakieleza masitiko yao, kuhusiana na Marekani kuendelea kutumia kura ya turufu kupinga usitishwaji wa vita kule Gaza, Umoja wa mataifa nao ukiituhumu Isreali kwa kutekeleza uhalifu wa kivita kule Gaza na kutaka kumaliza Wapelestina.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment