Trump kukutana na Mfalme Charles katika kasri la Windsor

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais wa Marekani, Donald Trump ameanza rasmi ziara yake ya pili ya kiserikali nchini Uingereza siku ya Jumatano ambako amepangiwa kuwa na mazungumzo muhimu ya kidiplomasia.

Mfalme Charles na familia ya kifalme watampokea Rais Trump atakapowasili katika kasri la Windsor, eneo la zamani na kubwa zaidi kwa makazi ya Wafalme wa Uingereza kwa takriban miaka 1,000, akikaribishwa na msafara wa magari, maonyesho ya ufyatuaji risasi, maonyesho ya ndege za kijeshi na karamu ya kifahari.

Uingereza inasema itakuwa sherehe kubwa zaidi ya kijeshi ya makaribisho kwa ziara ya serikali katika kumbukumbu yake.

Trump, ameweka historia kwa kuwa kiongozi wa Marekani lakini pia mwanasiasa wa kwanza kualikwa na Mfalme wa Uingereza mara mbili.

“I Love King Charles,” aliweka ujumbe huo kwenye akaunti yake ya Truth Social mnamo mwazi Februari. Aliongeza alipowasili: “Nina mambo mengi hapa ambayo … yanauchangamsha moyo wangu. Ni mahali maalum sana.”

Washawishi wa TikTok wakamatwa kwa kumtusi rais wa Somalia

.

Polisi nchini Somalia wamewakamata wafuasi wanne wa TikTok kwa madai ya kumtusi Rais Hassan Sheikh Mohamud kwenye video ya densi.

Katika chapisho hilo vijana kadhaa wanaonekana wakicheza wimbo mpya wa kampeni uliotumika awali wakati wa kuwania urais mwaka wa 2022, lakini maneno hayo yakiwa yamebadilishwa na kujumuisha lugha ya

Katika taarifa, polisi walisema washukiwa hao wako kizuizini na watafunguliwa mashtaka rasmi. Hawajazungumza lolote tangu kukamatwa kwao.

Washawishi kadhaa wa mitandao ya kijamii wamekamatwa na kufungwa jela hapo awali kwa kueneza matusi yanayotokana na koo, uchochezi au maudhui “ya uasherati” kwenye majukwaa kama vile TikTok – lakini hii ni kesi ya kwanza inayohusisha mwanasiasa mkuu.

Iran yamhukumu kunyongwa mtu anayetuhumiwa kufanya ujasusi wa Israel

Woman With Israeli Flag

Iran imemhukumu kunyongwa mtu aliyetuhumiwa kufanya ujasusi kwa ajili ya Israel, kulingana na ripoti kutoka kwa vyombo vya habari vya serikali siku ya Jumatano aliyetambulishwa kama Babak Shahbazi.

Iran imetoa hukumu ya kifo kwa watu wengi inaowatuhumu kuwa na uhusiano na idara ya kijasusi ya Israel ya Mossad na kuwezesha shughuli zake nchini humo.

Visa vya hukumu ya kunyongwa kwa Wairani waliopatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa ajili ya Israel vimeongezeka kwa kiasi kikubwa mwaka huu, huku takriban hukumu tisa za vifo zikitekelezwa katika miezi ya hivi karibuni.

Vyombo vya habari vya serikali vilisema Shahbazi alifanya kazi na Esmaeil Fekri, mfungwa mwingine aliyenyongwa mwezi Juni kwa kufanya ujasusi wa Israel tangu mapema 2022.

Shahbazi alishtakiwa kwa kutumia wadhifa wake kama mwanakandarasi anayeweka vifaa vya kupozea ili kukusanya taarifa kutoka sehemu nyeti na vituo vinavyohusishwa na jeshi na vyombo vya usalama.

Wakili wa mshtakiwa alikuwa ameomba kukata rufaa kwa Mahakama ya Juu Zaidi, ambayo ilikataa ombi hilo.

Kenya yamfungulia mashtaka Feisal ya biashara za pembe za faru aliyefungwa jela 2018 kwa kusafirisha pembe za ndovu

.

Mahakama ya Kenya jana Jumanne ilimshtaki mwanamume mmoja kwa biashara ya pembe mbili za faru zenye thamani ya shilingi milioni 8.2 za Kenya (dola 63,000), miaka tisa baada ya kufungwa jela kwa kusafirisha pembe za ndovu.

Feisal Mohamed Ali na mshukiwa mwenzake Mohammed Hassan walikamatwa katika mji wa bandari wa Mombasa mwezi uliopita.

Siku ya Jumanne, wawili hao walikana shtaka la kuhusika na wanyamapori walio hatarini kutoweka.

Ali aliachiliwa baada ya kukata rufaa mwaka wa 2018, miaka miwili ndani ya kipindi cha miaka 20 alichohukumiwa kwa ulanguzi wa pembe za ndovu, kutokana na dosari za utaratibu katika kesi hiyo.

Polisi walikuwa wamemshutumu kwa kuhusika na kundi la kimataifa la uwindaji haramu lililohusishwa na kunaswa kwa meno 120 ya ndovu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment