Sudan Kusini: Upinzani wataka kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi wa sasa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Upinzani nchini Sudan Kusini, umetoa wito wa uhamasishaji kwa wafuasi na vikosi vyake kujitayarisha kufanya mabadiliko ya uongozi wa serikali, ili kujibu mpango wa serikali wa kutaka kumfungulia kiongozi wake Riek Machar, mashtaka ya uhaini.

Rais wa Sudan Kuisni Salva Kiir na makamu wake Riek Machar
Rais wa Sudan Kuisni Salva Kiir na makamu wake Riek Machar AFP – PETER LOUIS GUME

Kupitia taarifa kaimu mwenyekiti wa chama cha upinzani, Oyet Nathaniel Pierino, amewataka wafuasi na kitengo cha jeshi la upinzani kujitayarisha kupigania mabadiliko  ya serikali, Oyet akidai serikali ya rais Salva Kiiri inatawala kwa mkono wa chuma na hilo sharti likomeshwe.

Juma lililopita makamu wa Kwanza wa rais Riek Machar, alifunguliwa mashtaka ya uhaini, uhalifu wa vita na mauwaji na kuondolewa wadhifa wa makamu wa Kwanza wa rais, hii ni licha ya kuendelea kuzuiliwa nyumbani kwa muda sasa.

Makamu wa Rais nchini Sudan Kusini.
Makamu wa Rais nchini Sudan Kusini. AP – Denis Farrell

Kesi dhidi ya Machar inatokana na wapiganaji wa White Army kuvamia kambi ya kijeshi na kuwaua zaidi ya wanajeshi 250, Machar akitumiwa kuhusika kwani wapiganaji hao wanatoka katika kabila lake la  Nuer, tuhuma ambazo Machar na washirika wake wamekanusha vikali.

Ushirikiano kati ya rais Salva Kiiri na hasimu wake wa jadi wa kisiasa Reik Machar unatishia kulitumbukiza tena taifa hilo kwenye vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo tayari vimewahi sababisha vifo vya watu laki 400 miaka ya awali.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment