Rushwa iliyokithiri Sudan Kusini inatishia ustawi wa taifa hilo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, yatoa wito kwa idara za uchunguzi nchini Kenya, kuchunguza tuhuma za rushwa na utakatishaji fedha dhidi ya makamu wa rais Benjamin Bol Mel. 

Rushwa iliyokithiri Sudan Kusini inatishia ustawi wa taifa hilo
Rushwa iliyokithiri Sudan Kusini inatishia ustawi wa taifa hilo © Emmanuel Makundi

Aidha tume hiyo, imesema hali ya rushwa na ubadhilifu wa fedha za uma nchini humo imefikia hatua mbaya ambayo inaweza kuitumbukiza tena nchi hiyo kwenye mzozo mwingine wa kisiasa.

Kwa mujibu wa wa mwenyekiti wa tume hiyo, Yasmin Sooka, uchunguzi wao umebaini ofisi ya Rais Salva Kiir kutumia kiwango kikubwa cha fedha kuliko hata bajeti inayotolewa kwenye wizara.

Sook ameongeza kuwa, kati ya mapipa ghafi ya mafuta yanayopatikana kwenye taifa hilo, ni pipa moja tu ndilo linaingia kwenye mfuko wa serikali, akihoji ni wapi mapipa 39 yamepelekwa.

Kwa upande wake, mjumbe wa tume iliyochunguza hali ya rushwa kwenye taifa hilo, Barney Afako, uteuzi wa upendeleo katika nafasi za juu serikalini, ikiwemo kupandishwa vyeo kiholela kwa majenerali wa jeshi, kumechangia hali kuwa mbaya.

Afako ametolea mfano fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara zinazounganisha mji mkuu wa Juba, kuwa ni barabara moja pekee ambayo inaelekea kukamilika katik ya tatu zilizokuwa zijengwe awali, huku fedha zilizotengwa zikiwa hazijulikani zilikopelekwa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment