Mungu Amemuandaa Huyu KUKUINUA…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kila mtu Huja MAJIRA anahitaji KUVUSHWA salama.

Ni hivi, kuna wakati utapitia MAUMIVU MAKALI sana ambayo watu wengi hawatayajua au watayapuuzia.

Itakuwa kama hakuna mtu anayejali, Kwenye kipindi hiki kuna mtu huwa ameandaliwa AKUVUSHE.

Si unajua kuna watu walipitia kipindi ambacho HAWAKUWA na kazi wala PESA, lakini hawakulala NJAA?

Kuna mtu aliinuliwa KUWAVUSHA.

Wapo ambao walipata STRESS za kutisha Kutokana na changamoto za KIMAHUSIANO ambazo walizipitia, akatokea MTU MMOJA wa KUWAVUSHA.

Nimeshakutana na mtu ambaye alikuwa MGONJWA na mwenye Madeni na akainuka mtu wa kusimama naye hadi akavuka salama na KUINUKA TENA.

Hata wewe, kwa chochote UNACHOPITIA LEO, usihitimishe kuwa hakuna mtu.

Endelea KUMUAMINI MUNGU, atakuinulia mtu wa KUSIMAMA na KUVUKA na wewe.

Ila Kumbuka, hao nao ni binadamu, watakukosea wakati mwingine, pamoja na yote USIJE KUSAHAU Wema wao Kwenye maisha yako.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment