Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wabunge wa Rwanda, Jumatatu ya wiki hii walipitisha azimio kulaani wito wa hivi karibuni wa bunge la umoja wa Ulaya lililoitaka serikali ya Kigali, kumuachia huru bila masharti, mwanasiasa Victoire Ingabire.

Kulingana na wabunge hao, hatua ya Umoja wa Ulaya inaiingilia mfumo wa mahakama wa Rwanda pamoja na kukiuka uhuru wa taifa hilo la Afrika Mashariki.
Ingabire alikamatwa mwezi Juni mwaka huu akituhumiwa kutegeneza kikosi cha kigaidi kwa malengo ya kuchochea vurugu.

Kufuatia tuhuma hizo, Umoja wa Ulaya katika maazio yake ya tarehe 11 ya mwezi huu, ulisema mashtaka dhidi ya mwanasiasa huyo yamechochewa kwa misingi ya kisiasa, ukiitaka Rwanda kuyaondoa mara moja.
Hii si mara ya kwanza kwa Ingabire kushtakiwa na Kigali ambapo mwaka wa 2013 alifungwa jela miaka 15 kwa makosa ya kuchochea uasi kabla ya kuachiwa mwaka wa 2018 kwa msamaha wa Rais.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.