“Breaking Point”.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwenye Maisha kuna wakati huwa unaitwa “Breaking Point”.

Kwa Mujibu wa Mwandishi maarufu wa vitabu Lisa Gupta, anasema kuwa “ Everyone has a breaking Point, No matter, how strong they are”: Akimaanisha bila kujali una Nguvu/Uhodari wa kiasi gani lazima utapitia wakati huu.

Huu Ni wakati ambao unaona Nguvu zimekuishia na hakuna tumaini tena,

Una maumivu makali ya Ndani na hauoni sababu ya kuishi tena,

Unatafakari na unaona uwekezaji na nguvu zote ulizoweka kwa Miaka mingi zinapotea bure,

Unaona Giza na hauoni namna unaweza kutoka, ni Kama umebaki peke yako,

Una madeni yanakuandama na yamekupa stress kiwango cha Juu,

Kuna kitu kimetokea na kimekupa aibu hautamani sura yako ionekane tena, unatamani kupotea usionekane.

Mtu wako wa Ndani AMEUMIA na AMEJERUHIKA, unahisi KUCHOKA.

Kila SHUJAA LAZIMA APITIE hali hii kabla hajaitwa shujaa.

Mbegu ili IOTE lazima kwanza IFE. Kuna MAJIRA lazima UPITIE ambayo inaweza kuonekana kuwa ndio umefika mwisho, kumbe ni mchakato muhimu unapitia kabla ya KUOTA.

.

Kama mbegu ingepewa uchaguzi wa kuamua basi isingetaka KUFUKIWA chini kabla haijaota, ingetamani iote ikiwa juu, hata hivyo haiwezekani.

.

Kuna mtu ambaye leo ukijiangalia unaona kama NDOTO, MALENGO na MAISHA yako yamefikia TAMATI kwa sababu umekuwa kama mbegu iliyofukiwa: Hakuna mwanga, hakuna anayekuona na kukutambua n.k USISAHAU kuwa huo ni mchakato ili UOTE.

.

Kuna wakati mbegu inatamani iingekaa muda mfupi chini ya ardhi ili ITOKEE JUU ila ni lazima ISUBIRI. Nawe pia, najua unatamani kutokea kwa JUU HARAKA.

.

Kuna watu wakikuangalia leo wanadhani ndio umefika mwisho, HAWAJUI uko kwenye mchakato, wakati wanahesabu kuwa UMESHAPOTEA watashangaa HUYO UNACHIPUA.

.

Wewe ni MBEGU kuna SIKU UTACHIPUA.

Ufanye nini: Make Your Breaking Point To Be Your Turning Point. Ukiona hali hii ujue unaingia MSIMU MPYA wa MAISHA YAKO.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment