Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mshukiwa Tyler Robinson, 22, aliwekwa kizuizini saa 33 baada ya Kirk, mwanaharakati wa mrengo wa kulia mwenye umri wa miaka 31, kuuawa kwa kupigwa risasi huko Orem siku ya Jumatano.
Akizungumza na ABC News, Cox, wa Republican, alisema watu walio karibu na Bw Robinson wamekuwa wakishirikiana na uchunguzi huo.
Cox alionekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya Marekani Jumapili asubuhi, ambapo pia alisisitiza wasiwasi kuhusu mitandao ya kijamii baada ya kifo cha Kirk.
Gavana huyo pia aliulizwa kuhusu ripoti ya New York Times iliyodai kuwa Bw Robinson alizungumza na wengine baada ya kupigwa risasi kupitia jukwaa la ujumbe la Discord, ikiwa ni pamoja na madai kwamba alitania kuwa mshambuliaji.
Cox aliiambia ABC News: “Tunachoweza kuthibitisha ni kwamba mazungumzo hayo kwa hakika yalikuwa yakifanyika, na hawakuamini kuwa alikuwa yeye.
“Ilifanyika, yote yalikuwa mzaha hadi, hadi yeye, alipokubali kuwa ni yeye.”
Bw Robinson alikamatwa Alhamisi usiku baada ya kujisalimisha kwa polisi.
Viongozi wa Kiarabu wakusanyika kwa mkutano wa dharura huko Qatar

Mkutano wa dharura wa viongozi wa Kiarabu unafanyika huko Qatar leo kujibu shambulizi la Israeli kwa viongozi wa Hamas huko Doha wiki iliyopita.
Sehemu ya azimio la rasimu iliyoonekana na shirika la habari la Reuters lilisema shambulio la Israeli huko Qatar, pamoja na vitendo vya uadui na mauaji ya kimbari, kikabila, na njaa, yanatishia matarajio ya amani na kuishi pamoja kwa amani.
Awali, Waziri Mkuu wa Qatari, Sheikh Al Thani, alihimiza jamii ya kimataifa kuacha kuwa na upendeleo na kuadhibu Israeli.
Rais Trump alisema Qatar ni mshirika mkubwa wa Marekani na kwamba Israeli inapaswa kuwa mwangalifu kabla ya kufanya shambulio lolote.
Shambulio la Israeli lilitokea saa kadhaa baada ya Waziri wa Mambo ya nje wa Israeli, Gideon Saar kudai Israeli wamekubali pendekezo la Trump, ambalo lingewaachilia mateka wote 48 walioshikiliwa na Hamas huko Gaza kwa mabadilishano ya wafungwa wa Palestina walioshikiliwa na Israeli na kusitisha mapigano.
Israeli iliwauwa wanachama watano wa Hamas na afisa wa usalama wa Qatar katika shambulio hilo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kwa kauli moja shambulio hilo.
WHO yasema chanjo ya Ebola imeanza kutolewa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo

Shirika la Afya Dunia hapo jana Jumapili lilisema kuwa limeanza kutoa chanjo kwa wafanyikazi wa afya walio mstari wa mbele na waliokuwa na mawasiliano na watu walioambukizwa virusi vya Ebola katika Jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambapo mlipuko wa ugonjwa huo umetangazwa.
WHO imesema dozi 400 za awali za chanjo ya Ervebo Ebola kutoka akiba ya dozi 2,000 nchini humo zimefikishwa Bulape, kitovu cha mlipuko huo.
Kundi la Kimataifa la Kuratibu la Utoaji wa Chanjo limeidhinisha kutumwa kwa dozi 45,000 za ziada za chanjo ya Ebola nchini Congo, shirika hilo lilisema.
Mlipuko huo, wa kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka mitatu, ulitangazwa mapema mwezi Septemba.
Misitu minene ya kitropiki ya Congo ni hifadhi ya asili ya virusi vya Ebola, ambavyo husababisha homa, maumivu ya mwili, na kuhara, na vinaweza kukaa kwenye miili ya walionusurika na kuibuka tena miaka kadhaa baadaye.
Takwimu za hivi punde kutoka wizara ya afya huko Kinshasa zilisema kulikuwa na visa 32 vinavyoshukiwa, visa 20 vilivyothibitishwa na vifo 16.
Kudhibiti mlipuko huo “inawezekana, lakini itakuwa changamoto ikiwa tutakosa fursa hii,” Meneja wa Eneo la Mpango wa WHO Patrick Otim aliambia mkutano wa Geneva wiki iliyopita, akitoa wito wa kuungwa mkono zaidi kwa serikali na washirika wengine.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.