Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Unaijua kanuni ya VITA inayoitwa -“KANUNI YA MBWA WA NDANI?”. Kuna aina za changamoto ambazo ukizipitia fikra ya kwanza inayokuja ni “HAPA SITAWEZA KUCHOMOKA TENA”. Ni zile ambazo kila DALILI inayoonekana inaashiria kuwa hakuna njia ya kukutoa na kukupa USHINDI.
.
Sababu kubwa inayopelekea fikra hii kuwa na nguvu ni pale mtu anapolinganisha uwezo alionao,watu anaowafahamu au kiwango cha elimu na ukubwa wa changamoto.Ulinganifu huu humfanya mtu kukata tamaa na kujiona hawezi hasa pale anapoona kila alichonacho ni KIDOGO au KIDHAIFU ukilinganisha na UKUBWA wa CHANGAMOTO inayomkabili.
.
Kwenye maisha kuna kanuni muhimu sana ya vita inaitwa “Kanuni ya Mbwa wa Ndani”.Njia rahisi ya kuelezea kanuni hii ni kutumia maneno ya Mark Twain aliyesema ““It’s not the size of the dog in the fight, it’s the size of the fight in the dog”(Sio UKUBWA wa MBWA anayepigana BALI ni ukubwa wa DHAMIRA YA KUSHINDA iliyoko ndani ya MBWA ndio muhimu zaidi).
.
Kuna watu walipitia na wengine wanapitia kwenye changamoto kama zako,kinachotofautisha sio kwamba wao wana pesa nyingi,elimu kubwa,wanajuana na watu wengi au wamependelewa sana-HAPANA:Kinachotofautisha ni wao wameamua kutokea NDANI YAO KUWA HAWATAKUBALI kukata tamaa.
.
Kumbuka tatizo hilohilo linalowafanya wengine wajinyonge kuna wengine ndio linawapa USONGO wa maisha wa kutafuta zaidi, hilohilo ambalo linawafanya wengine WALAE ndani siku nzima wengine wanalitumia kutembea kila mahali kutafuta SULUHISHO,linalowafanya wengine WAJIKATAE ndio linawafanya wengine waweke NADHIRI ya KUVUNJA historia n.k
.
Mtu mmoja alipata shida nyingi na akarudi chini kimaisha sana,adui zake walipomcheka akawaambia “Hata kama kwa nje naonekana maskini,ndani yangu kuna mbegu ya utajiri, ITACHIPUA”-Na wewe unaweza kusema “Hata kama kwa nje naonekana nimeanguka,ndani yangu nimesimama na sitakubali kukata tamaa”.
.
Kumbuka kanuni hii-Bila kujali udogo wako au usichonacho: Cha muhimu ni dhamira ya ushindi iliyoko ndani yako.
Mbwa mdogo na MWEMBAMBA mwenye DHAMIRA ya NGUVU anaweza KUMSHINDA MBWA mkubwa na MNENE asiye na dhamira ya kushinda.UTASHINDA.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.