Face Your Fears Today.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna watu wengi sana ambao kama wangeongeza kiwango kidogo tu cha KUJIAMINI, basi dunia INGEWASHANGAA SANA…

Yamkini wewe ni miongoni mwao!

Hivi unajua kuna watu wana UWEZO MDOGO sana kuliko wewe…

…Ila wanafanya mambo MAKUBWA kuliko wewe?

Na sababu ni kwamba WANAJIAMINI💪 kuliko wewe!

Moja ya eneo unalotakiwa kujenga uwezo wako kwa bidii ni KUJIAMINI.

Yamkini kwa kukosa kujiamini UNAOGOPA KUMPIGIA MTU SIMU ambaye angekupeleka hatua inayofuata.

Una mawazo MAZURI ila huyafanyii kazi kwa sababu UNOGOPA UTAFELI n.k

Njia ya kwanza kabisa unayoweza kuitumia kujenga kujiamini,

Ni KUAMUA KILA SIKU KUFANYA JAMBO MOJA UNALOLIOGOPA ila ni la MUHIMU.

Hii ndio maana mwandishi nguli Mark Twain aliwahi kusema….

“Fanya lile unalolihofia, na hapo utaiua hofu”.

Kwamba (Do what you fear and the Death of Fear Is Certain).

Kuna hatu leo ambayo unatakiwa kuichukua.

Kila siku umekuwa unaghairisha.

LEO amua kumalizana nayo.

Hofu haiondoki kwa KUIKIMBIA ila inaondoka kwa KUIKABILI.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment