Mamlaka Tanzania yafungia Jamii Forum kwa siku 90

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.
Maelezo ya picha,Maxence Melo

Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na pia kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni

“Mnamo tarehe 04 Septemba 2025, JamiiForums kupitia jukwaa lake na akaunti zake za mitandao ya kijamii ilichapisha maudhui ya kupotosha Umma, kukashifu na

kudhalilisha Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na

Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020 na Marekebisho yake ya mwaka” ilisena taarifa hiyo ya TCRA.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Jamii Forum, inasema kuwa “TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuweka tarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa

Tanzania na “Mfanyabiashara” Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.

Kwa mujibu wa TCRA, JamilForums ilishindwa kutafuta

maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo)

zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za

upande mmoja.

Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment