Putin apinga mpango wa usalama wa mataifa ya Magharibi nchini Ukraine

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Putin anasema vikosi vyovyote vya kimataifa vitakavyopelekwa nchini Ukraine vitakuwa “lengo halali”

Rais wa Urusi Vladimir Putin amepinga pendekezo la nchi za Magharibi la “kupeleka jeshi” nchini Ukraine siku moja baada ya kusitishwa kwa mapigano, kufuatia mkutano wa kilele wa Paris unaolenga kukamilisha mipango ya dhamana ya usalama.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema washirika 26 wa Ukraine wamejitolea rasmi kupeleka wanajeshi wa “nchi kavu, majini au angani” kusaidia kudumisha usalama mara baada ya mapigano kusitishwa. Hakueleza kwa undani nchi yoyote iliyohusika.

Putin alitaka kukomeshwa kwa mpango huo, akionya kwamba wanajeshi wowote watakaopelekwa nchini Ukraine watakuwa “lengo halali”, haswa ikiwa watajitokeza muda huu, ingawa mpango wa kuwapeleka kwa sasa hujafikiwa.

Matumaini ya kusitishwa kwa mapigano kwa sasa yamefifia, baada ya mkutano wa kilele wa mwezi uliopita huko Alaska kati ya Putin na Rais wa Marekani Donald Trump kuibua kwa ufupi matumaini ya kiongozi huyo wa Urusi kukutana na mwenzake wa Ukraine na Volodymyr Zelensky na uwezekano wa makubaliano ya amani kufikiwa.

Putin alisema siku ya Ijumaa yuko tayari kwa mawasiliano na kiongozi huyo wa Ukraine “lakini sioni sababu ya kufanya hivyo kwa nini? Kwa sababu ni vigumu kufikia makubaliano na Ukraine kuhusu masuala muhimu”.

Msemaji wake, Dmitry Peskov, alisifu “juhudi” za Trump za kutatu mzozo wa Ukraine, na kuyashambilia mataifa ya Magharibi kwa “kuchochea kuendelea kwa vita”.

Thailand yamchagua waziri mkuu wa tatu katika kipindi cha miaka miwili

Anutin ni waziri mkuu wa tatu wa Thailand katika kipindi cha miaka miwili
Maelezo ya picha,Anutin ni waziri mkuu wa tatu wa Thailand katika kipindi cha miaka miwili

Bunge la Thailand limemchagua mfanyabiashara Anutin Charnvirakul kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo – wa tatu katika kipindi cha miaka miwili, baada ya kiongozi mwingine kuondolewa madarakani.

Paetongtarn Shinawatra, aliondolewa madarakani na mahakama ya kikatiba wiki iliyopita kwa ukiukaji wa maadili juu ya jinsi alivyoshughulikia mzozo wa mpaka na Cambodia.

Chama cha Bhumjaithai cha Anutin kilijitenga na muungano unaoongozwa na Shinawatra wa Pheu Thai, na kupata uungwaji mkono wa kutosha bungeni na kushinda uwaziri mkuu.

Lakini msukosuko uongozini huenda isikome Thailand ambayo imeshuhudia tawala nyingi zikiondolewa kupitia uingiliaji wa mahakama na mapinduzi ya kijeshi katika siku za hivi karibuni.

Kungia madarakani kwa Anutin kni pigo kubwa kwa familia ya Shinawatra, ambayo imetawala siasa za Thailand tangu 2001, wakati babake Paetongtarn Thaksin alipokuwa Waziri Mkuu.

Wafanyakazi wa misaada watumia punda kuwafika waathiriwa wa maporomoko ya ardhi Sudan

.

Wafanyakazi wa misaada kwa kutumia usafiri wa punda wamefanikiwa kuwasilisha msaada wa kwanza wa kibinadamu kwa manusura wa maporomoko ya ardhi yaliyoripotiwa kuua mamia ya watu katika kijiji cha milimani huko Darfur magharibi mwa Sudan.

Mvua kubwa na mafuriko yaliyokumba kijiji cha Tarasin yalisababisha maafa siku ya Jumapili huku punda wakitumia kama njia pekee ya kufikia familia zilizoathiriwa.

“Familia huko Tarsin zimepoteza kila kitu. Iliwachukua wahudumu wetu zaidi ya siku kupitia njia yenye mawe, matope na milima kufikia wakaazi hawa walioathiriwa,” alisema Francesco Lanino, kutoka shirika la misaada la Save the Children.

Bado haijabainika ni watu wangapi walikufa.

Kundi lililojihami linalodhibiti eneo hilo linakadiria kuwa watu 1,000fariki katika maporomoko hayo, lakini wizara ya afya inasema ni miili miwili pekee ndio imepatikana.

Siku ya Alhamisi, viongozi wa raia wa eneo hilo walisema kuwa wameopoa na kuzika miili ya mamia ya watu.

Rubio asema Marekani ‘itayalipua’ makundi ya wahalifu wa kigeni

Rubio

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema nchini hiyo “italipua” makundi ya uhalifu ya kigeni ikihitajika, ikiwezekana kwa ushirikiano na mataifa mengine.

“Sasa watatusaidia kuwasaka watu hawa na kuwalipua, ikiwa ni hivyo,” Rubio alisema wakati wa ziara ya Ecuador.

Pia alitangaza kuwa Marekani itayaorodhesha magenge mawili makubwa ya wahalifu nchini Ecuador, Los Lobos na Los Choneros, kama mashirika ya kigeni ya kigaidi.

Kauli jiyo inakuja siku chache baada ya vikosi vya Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya boti moja katika bahari ya Caribbean.

Ikulu ya White House inasema iliwaua walanguzi 11 wa dawa za kulevya, lakini haikutoa utambulisho wao.

Usiku wa Alhamisi, idara ya ulinzi ilishutumu ndege mbili za kijeshi za Venezuela kwa kuruka karibu na meli ya Marekani katika “hatua ya uchochezi iliyopangwa kuingilia shughuli zetu za kukabiliana na ugaidi”.

Venezuela bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.

Marco Rubio alipoulizwa ikiwa wasafirishaji haramu kutoka nchi ambazo ni za washirika wa Marekani, kama vile Mexico na Ecuador, wanaweza kukabiliwa na majeshi ya Marekani.

Alisema “serikali rafiki” zitatusaidia kuwatambua wasafirishaji haramu. “Rais amesema anataka kupambana na makundi haya kwa sababu yamekuwa yakitushambulia kwa miaka 30 na hakuna aliyechukua hatua. “Lakini hakuna haja ya kufanya hivyo katika hali ambapo wahusika wanatoka katika nchi amayo ni mshirika wetu, kwa sababu serikali rafiki zitatusaidia.”

Serikali za Ecuador na Mexico hazijasema zitasaidia katika mashambulizi ya kijeshi.

Tetemeko la tatu la ardhi latokea Afghanistan huku idadi ya vifo ikiongezeka

.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.6 katika kipimo cha Richter lilikumba eneo la mbali la kusini-mashariki mwa Afghanistan usiku wa Alhamisi, likiwa ni tetemeko la tatu katika muda wa siku sita, huku idadi ya waliofariki kutokana na lile la kwanza ikiendelea kuongezeka.

Tetemeko hilo lilitokea saa 20:56 saa za eneo (15:36 GMT) na kusababisha watu katika majimbo ya Nangarhar na Kunar kutoroka kutoka kwenye makazi yao kwa hofu.

Hakukuwa na ripoti rasmi ya majeruhi kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Alhamisi usiku, lakini madaktari waliokuwepo eneo hilo waliambia BBC kuwa watu 17 waliojeruhiwa waliletwa katika Hospitali ya Mkoa ya Kunar.

Tetemeko la Jumapili limeua watu 1,368 na kujeruhi wengine 2,180, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OHCA) ilisema, ikinukuu ripoti kutoka vijiji 25.

Papa Leo XIV na rais wa Israeli wajadili ‘hali mbaya ya Gaza’

.

Papa Leo XIV na wanadiplomasia wake wakuu wamezungumza na rais wa Israeli siku ya Alhamisi na kumfahamisha kwamba suluhisho la serikali mbili ndio “njia pekee ya kumaliza vita” vya Gaza huku Vatican ikitaka usitishaji wa kudumu wa mapigano hayo, kuachiliwa kwa mateka wote na kuingia kwa misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina waliokumbwa na njaa.

Vatican ilitoa taarifa ya kina isivyo kawaida kufuatia mkutano wa Leo na Rais wa Israeli Isaac Herzog, ambaye pia alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.

Herzog, kwa upande wake, alisema alimwomba Leo kukutana na familia za mateka, na akatoa wito wa kuimarishwa juhudi za kimataifa ili kuwaachilia huru.

Papa Leo XIV alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mnamo mwezi Julai baada ya shambulizi la kigaidi la Israel kulivamia kanisa pekee la Kikatoliki huko Gaza na kuua watu watatu na kumjeruhi kasisi wa parokia hiyo.

Urusi yasema nchi za Magharibi haziwezi kutoa usalama kwa Ukraine

.

Urusi imekataa hali yoyote ambapo wanajeshi wa kigeni watapelekwa nchini Ukraine ili kuwahakikishia usalama, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi.

Hii inafuatia ahadi ya Emmanuel Macron kwamba washirika 26 wa Magharibi walijitolea rasmi kupeleka wanajeshi “kwa nchi kavu, baharini au angani” kwenda Ukraine siku moja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Baada ya mkutano wa kilele wa nchi 35 uliopewa jina la “Coalition of the Willing” yaani “Muungano wa Walio Tayari”, rais wa Ufaransa alisema uungwaji mkono wa Marekani utakamilika katika siku zijazo.

Rais Donald Trump hivi majuzi alidokeza kwamba uungwaji mkono wa Marekani “huenda” ukawa kwa njia ya usaidizi wa ulinzi wa angani, na Volodymyr Zelensky wa Ukraine alisema alikuwa amezungumza na kiongozi huyo wa Marekani kuhusu “ulinzi zaidi wa anga wa Ukraine”.

Joe Biden alifanyiwa upasuaji wa saratani ya ngozi

.

Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden amefanyiwa upasuaji wa saratani ya ngozi, msemaji wake amesema.

Haijulikani ni lini alifanyiwa upasuaji huo, lakini video ya mwishoni mwa Agosti ilionyesha akitoka kanisani huko Delaware akiwa na kovu kubwa jipya kichwani.

Msemaji huyo aliambia mshirika wa Sky News Marekani, NBC News, kwamba alikuwa anaendelea kupata afueni.

Upasuaji wa Biden ulihusisha kuondoa safu ya tishu, kuichunguza chini ya darubini ili kuona ikiwa kuna chembechembe za saratani zilizosalia, na kurudia ikiwa kutakuwa na lazima ya kufanya hivyo.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 82 alikuwa na ‘basal cell carcinoma’, mojawapo ya aina mbili za saratani ya ngozi, iliyoondolewa kifuani mwake mwaka wa 2023.

Daktari wake alisema wakati huo kwamba seli zote za saratani zilikuwa zimeondolewa.

Mwaka huo huo, mke wa Bw Biden, Jill, aliondolewa saratani mbili za ‘basal cell carcinomas’ karibu na jicho lake na kifuani mwake.

Rais huyo wa zamani pia alifichua mwezi wa Mei mwaka huu kwamba alikuwa na saratani ya tezi dume ambayo iko hatua ya nne – huku ugonjwa huo ukisambaa hadi kwenye mifupa.

Macron asema nchi 26 ziko tayari kutuma wanajeshi Ukraine

.

Washirika 26 wa Magharibi wamejitolea rasmi kupeleka wanajeshi “nchi kavu, baharini au angani” kwenda Ukraine siku moja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuafikiwa, Emmanuel Macron amesema.

Baada ya mkutano wa kilele wa nchi 35 uliopewa jina la “Coalition of the Willing” yaani “Muungano wa Walio Tayari”, rais wa Ufaransa alisema uungaji mkono wa Marekani kwa “jeshi lao” utakamilika katika siku zijazo.

Rais Donald Trump hivi majuzi alidokeza kwamba uungwaji mkono wa Marekani “huenda” ukaja kwa njia ya usaidizi wa anga, na Volodymyr Zelensky wa Ukraine awali alisema alikuwa amezungumza na kiongozi huyo wa Marekani kuhusu “ulinzi zaidi katika anga ya Ukraine”.

Matumaini ya makubaliano ya kumaliza mapigano ya Ukraine yamefifia tangu Vladimir Putin wa Urusi kukutana na Trump huko Alaska mwezi uliopita.

Trump alisema EU inapaswa kushirikiana na Marekani kusitisha uagizaji wa mafuta na gesi ya Urusi, kusitisha “kampeni za kivita za Urusi kwa njia za kiuchumi”, kulingana na mazungumzo ya simu kutoka kwa Rais wa Ufini Alexander Stubb.

Uswidi yaishutumu Urusi kwa msongamano wa mawimbi ya GPS kwenye Bahari ya Baltic

,

Uswidi imeishutumu Urusi kwa kuchangia ongezeko kubwa la visa vya msongamano wa mawimbi ya GPS (yaani mfumo wa kupokea taarifa kutoka kwenye setilaiti) katika Bahari ya Baltic, na hivyo kuzua wasiwasi wa usafiri wa anga katika eneo hilo.

Shirika la Usafiri la Uswidi (STA) lilisema ripoti za usumbufu zimeongezeka katika miaka michache iliyopita, lakini sasa imekuwa tukio la karibu kila siku. Ilirekodi matukio 733 kufikia sasa katika mwaka wa 2025, kutoka 55 katika mwaka mzima wa 2023.

Shirika hilo lilisema chanzo cha mwingiliano huo kilipatikana katika eneo la Urusi, na pia kuathiri usafirishaji wa meli. Mataifa mengine ya Ulaya yameishutumu Urusi kwa kuhusika na msongamano huo, jambo ambalo Moscow inakanusha.

Ripoti ya STA inajiri siku chache baada ya ndege iliyokuwa imembeba Ursula von der Leyen kukumbwa na hali hiyo.

Magwiji wa ndondi Mike Tyson na Floyd Mayweather kukutana ulingoni 2026

.

Magwiji wa ndondi Mike Tyson na Floyd Mayweather kukutana ulingoni mwaka 2026, kulingana na kampuni ya ndondi ya CSI Sports.

CSI Sports tayari imetangaza pambano kati ya Tyson, ambaye atatimiza umri wa miaka 60 mwaka ujao, na Mayweather, 48, lakini haikutoa mahali au maelezo yoyote ya tarehe, zaidi ya kusema kwamba pigano hilo lifanyika mwaka ujao.

Bingwa wa zamani wa uzani wa juu duniani Tyson, ambaye alipoteza pointi kwa Jake Paul katika pambano la raundi nane mnamo Novemba 2024, alisema: “Pambano hili si jambo ambalo ulimwengu wala sikuwahi kufikiria lingetokea au lingeweza kutokea.

“Ndondi imeingia katika enzi mpya ya kutotabirika – na pambano hili halitabiriki kabisi.

“Bado siamini kwamba Floyd anataka kufanya hivi. Itakuwa hatari kwa afya yake, lakini anataka kufanya hivyo, kwa hivyo imesainiwa na itafanyika.”

Mayweather alishinda mataji ya dunia katika aina tano ya viwango vya uzito tofauti bila kushindwa katika maisha yake ya mapambano 50 ambayo yalimalizika kwa ushindi dhidi ya nyota wa MMA Conor McGregor mnamo 2017.

.

Mshirikishe mwenzako, Magwiji wa ndondi Mike Tyson na Floyd Mayweather kukutana ulingoni 2026

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment