USIWACHUKIE, KUWATUKANA ama KUWANENEA MABAYA.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Taasisi ya utafiti ya chuo kikuu cha Stanford waliwahi kufanya utafiti ili kujua nini hasa kinachangia mafanikio ya mtu.

Katika utafiti wao walihitimisha kuwa, maarifa huwa yanachangia 12.5% na 87.5% inachangiwa na uwezo wako wa kuhusiana na watu.

Hii ndio maana bilionea wa kwanza kabisa kutokea Marekani, John D Rockfeller aliwahi kusema.

“Nitamlipa zaidi mtu ambaye anaweza kuhusiana na watu katika kazi yake kuliko mtu mwingine yeyote yule”.

Uwezo wa kuhusiana na watu ni pamoja na kutawala hisia zako pale ambapo wamekuudhi.

Kuna wakati mtu/watu watasema au kufanya kitu ambacho ukiamua kufanya kitu cha ajabu hakuna atakayeshangaa, ila unaamua kudhibiti hasira zako.

Uwezo unaozungumzwa hapa ni pamoja na kutokukubaliana na wengine ila USIWACHUKIE, KUWATUKANA ama KUWANENEA mabaya.

Ni kuelewa kuwa watu wote hatuwezi kuwaza sawa, hivyo kukubali kuheshimu mawazo ya wengine hata kama haukubaliani nayo.

Asilimia 87.5 inajumlisha uwezo wako wa kuchambua kinachozungumzwa na kushambulia HOJA badala ya kumshambulia MTOA HOJA.

Leo, jipime una asilimia ngapi katika kudeal na watu?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment