Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ukisoma historia za watu waliofanikiwa utashangaa kuona wengi walijaribu mara nyingi sana kufanya kitu fulani hadi wakafanikiwa.
Kuna watu huwa wanakata tamaa haraka sana.
Yaani akifanya biashara akipata hasara tu anakata tamaa jumla.
Kuna watu akijaribu kuomba kazi asipoitwa mara kadhaa, anakata tamaa.
Kuna wengine hadi wanaanza kusema kuwa wao wanaandamwa na mikosi fulani.
Kumbuka siku zote, Dunia huwa inatabia ya kuruhusu wale tu ambao wako serious na wanachotaka ndio wafanikiwe.
Dunia inajuaje mtu yuko serious?
Ni pale inapoona haukubali kuishia njiani, unapambana hadi kieleweke bila kuchoka.
Unayakumbuka maneno ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Margareth Thatcher
“You May Have To Fight A battle More than Once to Win It”
Kuna wakati utahitaji kupigana vita zaidi ya mara moja ili ushinde.
Ni kweli ulijitoa na ukapambania ndoto yako ila haikutokea.
Anzisha mapambano upya.
Kumbuka, USICHOKIPIGANIA kwenye maisha HAUTAKIPATA.
Kama unataka nikusaidie kujifunza Namna ya kuibuka mshindi katika ya nyakati ngumu.
“Jinsi Ya Kuibuka Mshindi Katikati Ya Nyakati Ngumu”.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.