Mambo Matatu Muhimu Ya Kukusaidia Kuwa na Furaha Kila Siku.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

1. HISIA IMARA (Emotional Stability)

Kila wakati kuna matukio na watu ambao watakuwa wanafanya mambo ya kukuumiza/kukuhuzunisha ama kukuvunja moyo.

Ukiwa mtu ambaye kila KINACHOTOKEA na KILA KINACHOSEMWA kinakuumiza na kufanya usiendelee, utaishia njiani.

Jifunze kuwa IMARA katika HISIA ZAKO na usiruhusu tukio/Mtu mmoja akufanye UACHE KABISA kufukuzia NDOTO ZAKO.

2. KUJITAFUTA UPYA (Identinty re-engineering)

Kuna mara kadhaa utadhamiria kufanya jambo fulani lakini baadaye MATUKIO ya MAISHA, FURSA, KUJITAMBUA upya n.k kunaweza kukufanya ubadilishe mwelekeo.

Kuna watu wamefanikiwa katika biashara ambazo mwanzo hawakuwa wamezifikiria.

Kuna watu walidhani watazeeka wakifanya Kitu fulani lakini leo wamejikuta wamefanikiwa kwenye Kitu kingine.

Kumbuka mipango yako ya leo inategemea unachokiona, usiogope kutumia fursa mpya zinazokuja.

Cha Muhimu ni kuwa kwa chochote unachofanya:

Focus, Consistency na Competency.

(Usiyumbishwe, Uwe na Mwendelezo na Jenga Uwezo)

3. KUFANYA, KUFANYA, KUFANYA (BE ON THE MOVE)

Kuna wakati hautajisikia kufanya, wewe amua KUFANYA.

Kuna wakati kila dalili itaonesha hausogei hatua, wewe fanya.

Moja ya MAAMUZI unatakiwa kuyafanya MAISHA YAKO yote ni kuwa UTAENDELEA KUFANYA kila siku bila kujali vizuizi.

USIPIME siku yako kwa MATOKEO peke yake, IPIME pia kwa MBEGU UNAZOPANDA ambazo kesho zitatoa MATUNDA.

Usikubali siku ipite haujafanya Kitu hata kama ni kidogo sana.

Nakutakia mafanikio.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment