Unatumia mbinu ipi kumshinda adui.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwenye VITA huwa kuna mbinu nyingi sana za KUMSHINDA ADUI yako.

Ila kuna mbinu ukiona adui yako anazitumia ujue AMEANZA KUSHINDWA.

DALILI mojawapo ya mshindani wako kuanza kuishiwa nguvu ni pale…

…anapoanza KUSHINDWA kwenye HOJA na anaanza KUSHAMBULIA mambo BINAFSI.

Anapoanza kushambulia mambo ambayo ni ASILI kwako.

Anapoanza kukushambulia kwa sababu ya JINSIA yako au KABILA lako…

Anapoanza kushambulia DINI yako au RANGI yako:

Hapo ujue adui yako nguvu zimeanza KUMUISHIA.

Kwa mujibu wa mwalimu Nyerere alisema…

Njia nzuri ya kushughulika na mtu wa namna hii ni “Kumpuuza”, yaani kutomjibu.

Usisahau kuwa NGUVU YAKO haionekani kwenye MANENO yako tu…

….bali pia nguvu yako inaonekana kwenye UKIMYA WAKO wa KUPUUZIA usichopaswa KUJIBU.

Kama vile ambavyo UKINYAMAZA unapopaswa KUONGEA utakuwa unakosea…

…ndio hivyo hivyo UKIONGEA unapopaswa KUNYAMAZA utakuwa UNAKOSEA.

UMECHOSHWA na hali uliyonayo?

Uko SERIOUS Unataka nikusaidie KUTIMIZA MALENGO YAKO?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment