Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mambo yanapokuwa MAGUMU katika maisha,DHORUBA zinapoongezeka na CHANGAMOTO zinapozidi: Katika hali ya kawaida kila mtu anatarajia USEME na UFANYE mambo yatakayoonyesha kuwa na wewe UMEPANICK.
.
Kitu ambacho watu wengi sana wanasahau ni kuwa kupanick na HEKIMA huwa vinaenda katika mwelekeo UNAOPINGANA siku zote.Kadiri kiwango cha kupanick kinavyokuwa juu ndivyo kiwango cha hekima kinavvyozidi KUPUNGUA.
.
Moja ya NGUVU iliyojificha ndani ya mwanadamu inapatikana pale ambapo anaweza kudhibiti HOFU yake isizidi juu ya UWEZO wake wa kutawala HISIA ZAKE.
.
Badala ya kuanza KUSEMA na KUFANYA mambo kwa sababu ya hisia za kupanick,anza siku yako kwa UTULIVU wa AKILI.Pata dakika chache za kumuomba MUNGU Hekima juu ya tatizo linalokukabili na usifanye maamuzi kwa sababu ya HASIRA au KUKOMOA mtu.Kuna wakati utahitaji KUJIZUIA KUSEMA au KUFANYA hata kama watakuona mjinga.
.
Kuna watu wengi wanatarajia upanick kutokana na unayopitia,kuna wengine wanatarajia upoteze MWELEKEO au USEME na UFANYE mambo ya AJABU.Washangaze kwa kuwa tofauti na matarajio yao.
.
Anza siku yako kwa kujiambia: “Hata katika dhoruba hii,sitapanick na wala sitafanya maamuzi au kusema kitu nitakachokuja kujutia”.SITAPANIKI!
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.