Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muigizaji nguli wa Hollywood na aliyewahi kuwa Gavana wa Jimbo la California Nchini Marekani Arnold Schwarzenegger aliwahi kusema…
“Strength does not come from Winning, Your struggles develop strengths. When you go through hardships and decide not to surrender, that is strength“
“Ukomavu na Nguvu hazitokani na ushindi unaopata, Pale unapopitia CHANGAMOTO unakomaa, Pale unapopitia MAGUMU na ukaamua KUTOKATA TAMAA, hapo ndipo unapojijengea NGUVU na UKOMAVU”
Kila mtu huwa anatamani kuwa kama MASHUJAA au WASHINDI tunaowaona kila siku.
Hata hivyo ni muhimu kujua kuwa HAWAKUZALIWA HIVYO.
Walitengenezwa na MAGUMU waliyopitia.
MAGUMU unayopitia leo ndio yanakutengeneza kuwa mtu wa kipekee wa KESHO kama hautakata tamaa.
CHANGAMOTO unayopitia leo kama Utaamua kuwa HAUTAKA TAMAA, basi utavuka upande wa pili ukiwa MWENYE NGUVU ZAIDI.
Hauwi shujaa kwa kupitia mambo marahisi, unakuwa shujaa kwa kushinda mambo MAGUMU kama yanayokukabili leo.
Kama umependa makala hii tafadhali share na wengine.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.