Tofauti ya Umaarufu na kuwa Muhimu.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna mstari wa muhimu sana unaotenganisha kati ya mtu kutamani umaarufu (Popularity) na kuwa mtu wa muhimu (Significant).

Umaarufu ni kujulikana na wengi bila kujali unajulikana kwa lipi.

Hii ndio maana kwa kiu ya kutaka umaarufu mtu anaweza kufanya mambo ya aibu na ya kushangaza sana.

Kuna wengine wanautafuta umaarufu kwa sababu ya kiu tu ya kujulikana na wengine wana utafuta umaarufu ili watimize ndoto fulani.

Shida kubwa ya kutafuta umaarufu ni mtu kujikuta anafanya mambo ambayo yako kinyume na dhamira yake.

Na huwa wengi hawadumu kwani umaarufu ni kama upepo, unavuma na kupita.

Hii ndio maana inalazimika mtu wa namna hii afanye kitu kipya kila siku cha kumuongezea umaarufu.

Mtu mwenye umuhimu (Significant) ni yule anayefanya mambo yanayoongeza thamani katika wale wanaomzunguka na kila mtu anataka kumjua au kuwa karibu naye.

Hii inamaanisha umaarufu kwa mtu huyu ni matokeo ya umuhimu wake kwa watu.

Yaani anawaongezea thamani hadi wanajikuta wanamzungumzia na kutaka kuwa karibu naye.

Wakati kundi la kwanza hudumu katika AKILI za watu na ni rahisi kusahaulika hawa wa pili hudumu katika MIOYO ya watu na ni ngumu kusahaulika.

Wewe umewahi kukutana na watu wa kundi gani kati ya haya mawili?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment