Kampeni za uchaguzi mkuu Tanzania kuanza rasmi leo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu zinaanza rasmi leo, kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Mwanaharakati Boniface Mwangi, autaka urais Kenya

Mwangi

Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Kenya, Boniface Mwangi, ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kushiriki kwa kiasi kikubwa maandamano ya kupinga serikali, ametangaza Jumatano kwamba atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2027.

Uamuzi wake utaonyesha iwapo uungwaji mkono mkubwa wa maandamano, hasa kutoka kwa vijana wa Kenya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, unaweza kutafsiriwa kuwa nguvu ya kisiasa kupitia kura.

Mwangi aliwahi kugombea ubunge mwaka 2017 kwa ajenda ya kupinga ufisadi, lakini hakufanikiwa. Kwa miaka mingi amejijengea sifa ya kuwa msemaji jasiri dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu ndani na nje ya Kenya. “Uongozi wetu umetufeli kwa njia nyingi.

Unalipa kodi ukitarajia huduma, kinyume chake unalazimika kutoa rushwa ili kupata huduma hizo hizo,” alisema wakati wa uzinduzi wa azma yake ya kugombea urais.

“Kwa hivyo tunaposimama hapa, ni lazima turudishe nchi mikononi mwetu.”

Mnamo Mei mwaka huu, Mwangi alifukuzwa nchini Tanzania baada ya kusafiri huko kushuhudia kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu. Aidha, mnamo Julai, mahakama ya Kenya ilimfungulia mashtaka ya kumiliki mabomu ya machozi na risasi moja iliyopatikana nyumbani kwake.

Alikana mashtaka hayo, akisema mamlaka hayana ushahidi na akaitaja kesi hiyo kama “aibu kubwa.”

Mahakama kuu kusikiliza kesi ya urais wa Mpina leo

Luhaga Mpina

Mahakama Kuu ya Tanzania leo inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi ya kupinga kuenguliwa kwa mgombea urais wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, hatua ambayo inaweza kubadili mwelekeo wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kesi hiyo imepewa kipaumbele kwa maombi ya dharura yaliyowasilishwa na ACT-Wazalendo, ikidai uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) uliomnyima nafasi ya kugombea, ni kinyume cha sheria na haki za kidemokrasia.

Kwa mujibu wa mawakili wa chama hicho, mahakama leo itasikiliza hoja za awali zenye lengo la kuamua kama zuio hilo lilikuwa la kisheria, ama ni uamuzi wa kiutendaji uliopita mipaka ya kikatiba.

Iwapo Mpina atashinda shauri hili, anaweza kurejeshwa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha urais na hivyo kuongeza ushindani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Lakini iwapo kesi hiyo itatupiliwa mbali, itathibitisha uchaguzi kufanyika bila ACT-Wazalendo kuwa na mgombea wa urais.

Kesi hii inafuatiliwa kwa karibu na wadau wa siasa, kwa kuwa itakuwa kipimo cha namna taasisi za kisheria zinavyoshughulikia migogoro ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu.

Kampeni za uchaguzi mkuu Tanzania kuanza rasmi leo

Rais Samia na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi

Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu zimeanza rasmi leo, kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Hata hivyo, uchaguzi huu unatarajiwa kutokuwa na hamasa ya mshikemshike baada ya chama kikuu cha upinzani kutangaza kutoshiriki, kikidai mfumo wa uchaguzi wa sasa unakinufaisha chama tawala na hautoi usawa wa ushindani.

Kwa mujibu wa INEC, jumla ya vyama 18 vilivyosajiliwa vitashiriki uchaguzi huu, vikiwa na wagombea 17 wa urais.

Hali hiyo inatokana na mgombea wa urais wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, kutoidhinishwa kugombea baada ya Tume kubaini uteuzi wake ulikuwa kinyume cha taratibu.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa pia ilimwengua rasmi kufuatia pingamizi lililotolewa na mwanachama wa chama hicho, Monalisa Ndala. Sababu kuu iliyoelezwa ni kwamba Mpina alipata uanachama wa ACT-Wazalendo mnamo Agosti 5, 2025, nje ya muda wa kisheria wa kuchukua fomu za kugombea ndani ya chama, ambao ulipaswa kuwa kabla ya Mei 25, 2025.

Hali hii imesababisha chama hicho kushindwa kushiriki katika nafasi ya urais mwaka huu.

Hata hivyo chama hicho kimekwenda Mahakamani kupinga uamuzi wa Msajili na Tume. Kwa upande wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga kuzindua rasmi kampeni zake Agosti 28, 2025 katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.

Samia Suluhu Hassan, ataongoza uzinduzi huo akifuatana na mgombea mwenza wake, Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Uzinduzi huo utaashiria mwanzo wa kampeni za CCM kwa nafasi za urais, ubunge na udiwani, huku chama hicho kitakuwa cha kwanza kuzindua kampeni zake tangu INEC ilipotangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa kampeni, Agosti 28, 2025.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment