Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Aliyekuwa naibu wa Rais nchini Kenya Rigathi Gachagua amesema kwamba atagombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2027.
Akizungumza kwenye runinga ya Citizen Jumanne usiku, Gachagua alisema amedhamiria kuwa kwenye debe, na kuongeza kuwa ana sifa na ujasiri wa kupata uugwaji mkono wa kutosha.
“Mimi ni mgombea wa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Nina sifa na nina uugwaji mkono. Natafuta uungwaji mkono zaidi na nitakuwa kwenye debe kama mgombea wa rais,” alisema.
Akijitetea kwa kwasababu ya pingamizi za kisheria zinazomkabili, Gachagua alisema katiba inatoa fursa kwa kila Mkenya kugombea wadhifa wa kuchaguliwa mradi tu machaguo ya kisheria hayajakamilika.
“Katiba inakuhakikishia haki ya kugombea wadhifa wa kuchaguliwa hata kama umehukumiwa, ikiwa haujamaliza machaguo yanayopatikana kisheria. Mahakama ya Juu Zaidi haijatoa uamuzi kuhusu kuondolewa kwangu madarakani,” Gachagua alisema kwenye runinga ya Citizen.
Ripoti yaonyesha mvutano kati ya jeshi la Mali na mamluki wa Wagner

Operesheni za kibinafsi za Urusi nchini Mali zimesababisha chuki ndani ya jeshi la taifa hilo la Afrika Magharibi na serikali ya kijeshi, na kupelekea mapungufu ya usalama na kushindwa kupata makubaliano yoyote ya madini, ripoti mpya imebaini.
Kundi la Wagner lilianza kufanya kazi nchini Mali baada ya jeshi, ambalo lilichukua madaraka katika mapinduzi mawili mnamo 2020 na 2021, kuondoa vikosi vya Ufaransa na Umoja wa Mataifa ambavyo vilikuwa vimehusika katika kupigana na waasi wa Kiisilamu kwa muongo mmoja.
Kundi la Wagner lilitangaza kuondoka kwake mnamo mwezi Juni, lakini Corps Africa, kikosi kinachodhibitiwa na Urusi, kilisema kitaendelea kuwepo.
Vikundi vya kutetea haki za binadamu ikiwa ni pamoja na Human Rights Watch lenya makao yake New York, mara kwa mara yamekuwa yakishutumu kundi la Wagner lenye kupigana pamoja na jeshi la Mali, kwa kutekeleza vitendo vya dhuluma na unyanyasaji dhidi ya raia.
Ripoti hiyo kwa kuzingatia mahojiano na maafisa kutoka kwa jeshi la Mali, shirika la ujasusi, wizara za fedha na madini, na kuchapishwa Jumatano, shirika lenye kufanya uchunguzi – liligundua kuwa Wagner pia imesababisha matatizo kwa jeshi na serikali ilioajiriwa kuunga mkono.
Kulingana na ripoti hiyo, wanajeshi wa Mali huchukia mamluki wa Urusi ambao “hupendelewa kwa huduma zingine”, kama vile kuhamishwa kwa ajili ya matibabu jambo ambalo huwa si rahisi kwa wengine kutokana na uhaba wa mafuta.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi na Wagner haikujibu mara moja maombi ya kutoa maoni yake.
Lil Nas X asema yuko sawa baada ya “siku nne za kutisha”

Lil Nas X amesema yuko sawa baada ya “siku nne zilizopita za kutisha” tangu alipokamatwa huko Los Angeles.
Mshindi huyo wa Grammy, anayejulikana kwa wimbo wake wa kufoka wa Old Town Road, alikamatwa siku ya Alhamisi baada ya maafisa wa polisi kusema kuwa aliwashambulia baada ya kumpata akitembea barabarani akiwa uchi. Alipelekwa hospitali kwa matibabu kukiwa na uwezekano wa kutumia madawa kupita kiasi.
Siku ya Jumatatu, rapper huyo mwenye umri wa miaka 26 alikana kosa la kumjeruhi afisa wa polisi na kukataa kukamatwa. Baadaye aliachiliwa baada ya kulipa dhamana ya $75,000 (£56,000).
Akiweka ujumbe kwenye Instagram siku ya Jumanne, aliwahakikishia mashabiki akisema: “Msichana wenu atakuwa sawa…” Aliongeza: “zilikuwa siku nne za kutisha zilizopita.”
Mashambulizi mapya yameripotiwa ndani ya Urusi

Video iliyoonekana na kuthibitishwa na timu ya BBC inaonyesha athari ya shambulio la ndege isiyo na rubani katika jiji la Urusi la Rostov-on-Don.
Video iliyoshirikishwa kwenye programu ya kutuma ujumbe ya Telegram inaonyesha jengo likiwaka moto baada ya ndege isiyo na rubani kuanguka na kuwaka moto.
Katika mji wa kusini wa Urusi wa Rostov-on-Don, karibu 200km (maili 125) kutoka eneo la vita la Ukraine, picha kadhaa zinaonyesha jengo likiwaka moto.
Mchambuzi mwandamizi wa mkoa Yuriy Slyusar, aliweka ujumbe kwenye telegraph, akidai ndege zisizo na rubani 10 zilidunguliwa usiku kucha.
Vyombo vya habari vya ndani vinasema jengo lililoharibiwa lilikuwa kwenye Njia ya Khalturinsky na picha na video ambayo imethibitishwa na BBC inaonyesha jengo linalowaka moto kwenye kona ya Mtaa wa Moskovskaya.
Video nyingine, iliyorekodiwa kutoka kwenye roshani ya mita 350 (futi 1,100) kuelekea mashariki, inaonyesha tukio lile lile.
Wakati huo huo, Urusi imefanya mashambulizi kwa kutumia ndege 95 zisizo na rubani aina ya Shahed na nyinginezo za aina mbalimbali usiku kucha, Jeshi la Wanahewa la Ukraine liliripoti.
Kulingana na data ya awali, ndege zisizo na rubani 74 za Urusi za Shahed na nyinginezo zilidunguliwa au kuharibiwa na ulinzi wa anga kaskazini, kusini na mashariki mwa nchi, Jeshi la Anga lilisema.
Athari iliyosababishwa na ndege hizo ilirekodiwa katika maeneo tisa.
Msafara wa Mpina wazuiwa getini INEC, aenguliwa rasmi

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimepokea kwa mshtuko na fadhaa barua ya Tume ya Uchaguzi kuwa mgombea wake wa urais asifike ofisi za Tume kwa ajili ya uteuzi.
Imesema maamuzi hayo si tu ni aibu bali yanaibua maswali mengi kuhusu uadilifu, umakini, uweledi na uhuru wa Tume iliyopewa dhamana ya kusimamia Katiba, sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza usimamizi wa uchaguzi Tanzania.
”Ni hatari kwa Tume na Demokrasia yetu ikiwa uamuzi huu wa kumtaka mgombea asirudishe fomu utabaki bila ya kufutwa na Tume yenyewe, kuendelea na uamuzi huu kutaongeza imaniiliyopo kwa umma kuwa Tume hii si huru na kuwa haiwezi kutenda haki” ilieleza sehemu ya taarifa ya ACT.
ACT imeiomba Tume iepuke mtego wa kuifanya itekeleze majukumu yake kinyume na mipaka ya kisheria na katiba.
Tume ya uchaguzi ilipokea nakala ya barua kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa akitengua uteuzi wa Luhaga Mpina kuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama hicho.
Awali Msajili wa Vyama vya Siasa alitangaza kuwa uteuzi wa Mpina kupitia chama chake hicho kipya, haujakidhi matakwa ya kikanuni, kufuatia pingamizi lililowasilishwa na mwanachama wa chama hicho, Monalisa Ndala.
Kwa mujibu wa malalamiko ya Monalisa aliyoyawasilisha kwa Msajili, mgombea huyo alikiuka sheria ya chama cha ACT Wazalendo kwa kutokuwa mwanachama wa chama hicho siku saba kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.
Monalisa anasema mwisho w akuchukua fomu za uteuzi ulikuwa mei 25, 2025, kabla ya Mpina kuwa mwanachama hivyo mgombea huyo alikuwa nje ya muda kimchakato wa kikanuni za kiuchaguzi.
“Mpina alipata uanachama wa ACT – Wazalendo Agosti 5, 2025, siku moja kabla ya kutangazwa kwenye Mkutano mkuu wa chama hicho wa Agosti 6, 2025, kinyume na kanuni zetu zinavyotaka”, hakukuwa na ushahidi wa kikao chochote cha chama kilichorekebisha ratiba rasmi ya kuchukua na kurejesha fomu’, ilisema sehemu ya taarifa ya Monalisa kuhusu uamuzi wa Msajili.
Katika uamuzi uliotolewa Agosti 26, 2025 Msajili alibainisha kuwa Mpina hakutimiza vigezo vya uanachama kwa mujibu wa kanuni za chama, akisema kuwa alijiunga ACT-Wazalendo nje ya muda uliopangwa na hivyo hakustahili kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho.
Wakati huo huo, vyombo vya habari Tanzania, ikiwemo Mwananchi imeripoti msafara wa Mpina kuzuiwa getini wakati ukiingia kurejesha fomu za kuwania kuteuliwa kugombea urais wa Tanzania.
Msafara huo ulifika saa sita mchana na kukutana na maafisa ulinzi wa Jeshi la Polisi waliowazuia kuingia kwenye ofisi za tume.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.