Watu Laki Tano warejea jijini Khartoum tangu jeshi kulidhibiti : UN

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Umoja wa Mataifa unasema, watu zaidi ya Laki Tano, wamerejea katika jiji kuu la Sudan Khartoum mwezi Julai, miezi minne baada ya jeshi kulidhibiti.

Jeshi la Sudan limekuwa likipambana na wapiganaji wa RSF kuudhibiti Mji wa Khartoum.
Jeshi la Sudan limekuwa likipambana na wapiganaji wa RSF kuudhibiti Mji wa Khartoum. AP

Tume ya Kimataifa inayoshughulika na wahamiaji, imesema kurejea kwa watu hao jijini Khartoum, ni sawa na ongezeko la asilimia 400 la watu wanaorejea katika jiji hilo.

Hatua hii inakuja, wakati huu jeshi likisema linaendelea na harakati la kulijenga upya jiji hilo ambalo tangu Aprili 2023, limekuwa kama uwanja wa mapambano kati ya wanajeshi na wanamgambo wa RSF wanaopambania madaraka.

Mbali na jiji kuu Khartoum, watu wengine zaidi ya Milioni mbili wamerejea katia makaazi yao kwa kipindi cha karibu mieizi tisa iliyopita kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa, nusu wakirejea katka jimbo la Al-Jazira.

Licha ya watu kuanza kurejea nyumbani, mapigano bado yanaendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, huku mamia wakiuawa katika siku za hivi karibuni katika mji wa El-Fasher, ambapo mpaa sasa maelfu ya watu wameuawa na mamilioni kuyakimbia makaazi yao, wakiwemo wengine waliokimbilia katika nchi jirani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment