Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirikishi la Usalama wa Chakula (IPC) litatoa taarifa baadaye kuhusu njaa katika Ukanda wa Gaza.
Chombo kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kinachohusika na ufuatiliaji wa usalama wa chakula, ambacho chenyewe hakitangazi rasmi njaa, kilisema mwezi uliopita kwamba “hali mbaya zaidi ya njaa” ilikuwa “ikishuhudiwa Gaza”.
Wizara ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas inasema watu 271 wamekufa kwa “njaa na utapiamlo” tangu tarehe 7 Oktoba 2023 – ikiwa ni pamoja na watoto 112.
Mashirika ya kibinadamu yametoa wito kwa Israel kuwezesha upatikanaji wa misaada zaidi katika Ukanda huo, na kuonya uhaba wa chakula na maji unaweza kuibuka na kuwa baa la njaa kubwa.
Israel imekanusha kuwa Gaza kuna njaa, huku Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akisema mapema mwezi huu kwamba “sera ya Israel wakati wote wa vita imekuwa ikizuia mzozo wa kibinadamu …”.
Ripoti hiyo mpya inakuja chini ya saa 24 baada ya Netanyahu kusema kuwa ameidhinisha mipango ya shambulio kubwa katika mji wa Gaza, licha ya upinzani mkubwa wa kimataifa na wa ndani.
WHO yaonya juu ya hatari ya joto kali mahali pa kazi

Wafanyakazi duniani kote wanahitaji ulinzi bora dhidi ya joto kali kwani mabadiliko ya hali ya hewa husababisha mawimbi ya joto ya mara kwa mara – hiyo ni hitimisho la ripoti mpya kutoka kwa Shirika la Afya Duniani na Shirika la Hali ya Hewa Duniani.
Ripoti hiyo inasema mamilioni ya wafanyikazi wanakabiliwa na joto kali inayoathiri afya na utendakazi wao. Inatoa wito kwa serikali, waajiri, na wafanyakazi kushirikiana ili kuandaa mikakati ya kukabiliana na hali hiyo.
Ingawa WHO imeonya mara nyingi juu ya hatari za kiafya za joto kali, hii ni ripoti yake ya kwanza tangu 1969 haswa juu ya joto kali kazini.
Mkurugenzi wa mazingira, hali ya hewa na afya wa WHO Rüdiger Krech alisema ugunduzi huo unapaswa kuwa tahadhari.
Miili mitano yafukuliwa karibu na Shakahola

Miili mitano imegunduliwa huko Kilifi kufuatia kumalizika kwa makaburi 6 katika kijiji cha Kwa Binzaro karibu na Shakahola katika mkoa wa pwani wa Kenya.
Hii inakuja baada ya ugunduzi wa makaburi yenye kuhusishwa na kanisa la ‘Kufunga hadi Kufa’ huko Shakahola lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 400 mnamo 2023.
Hussein Khalid, mwanaharakati wa haki za binadamu na Mkurugenzi Mtendaji wa Vocal Africa ambaye alikuwa kwenye maeneo ya makaburi alisema:
“Mwili wa kwanza ambao ulipatikana na wenyewe ulionekana kuzikwa hapo hivi karibuni wiki mbili hadi tatu zilizopita. Lakini minne inaonekana kuwa ilizikwa kitambo kidogo na ilikuwa katika hali ya kuharibika.”
Makaburi 21 yanatarajiwa kufukuliwa hii leo.
Kwa mujibu wa Bwana Khalid, kuchimbwa kwa kaburi la kwanza jana kulionyesha dalili za mchezo fulani unaoendelea.
“Hakuna mabaki yaliopatikana lakini ilionekana kana kwamba siku zilizopita, mtu, watu wengine au kundi fulani waliondoa maiti zilizokuwepo hapo. Ishara zilionyesha wazi kwamba kulikuwa na mwili eneo husika. Kitu pekee ambacho tulipata kutoka kaburi la kwanza kilikuwa nguo za ndani za wanawake na watoto. Hiyo ilionyesha kwamba inawezekana mtu au watu waliozikwa hapo walikuwa wanawake na watoto.”
Hayo yanajitokeza baada ya hofu kwamba ‘Kanisa la Kufunga hadi Kufa’ huenda nado linaendeleza shughuli zake licha ya Mchungaji wake Paul Mackenzie kuwa kuzuizini.
Mwezi uliopita, mahakama ya Kenya ilikuwa imeamuru kufukuliwa kwa miili inayoshukiwa kuwa ni ya watu ambao walikufa kwa njaa na kukosa hewa kaunti hiyo hiyo ambapo mamia ya washiriki wa kanisa la Mackenzie walipatikana miaka miwili iliyopita.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.