Unajifunza nini kutoka-Abraham Lincoln

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Abraham Lincoln aliwahi kuwa Rais wa Marekani, hata hivyo ni mmoja wa watu ambaye anashikilia rekodi ya kufeli mara nyingi sana kabla ya kufanikiwa kuwa Rais.

Siku moja baada ya kufeli mara kadhaa aliwahi kusema “I will prepare, and one day my time will come” (Nitajiandaa na siku moja muda wangu utafika).

Na kweli, kuna siku muda wake ulifika akatimiza ndoto yake.

Inawezekana una ndoto kubwa sana.

Inawezekana una mipango mikubwa sana kwenye maisha yako ila ukweli ni kuwa…

.

…kuna wakati hautapata unachotaka kwa haraka kama ulivyopanga.

Watu wengi wakifika wakati huu ndio huchoka na kuishia njiani.

Kumbuka, watu wanaofaidika na fursa ni wale ambao zinawakuta wamejiandaa.

Badala ya kulia, badala ya kulalamika au badala ya kujilinganisha na wengine…

.

…wewe amua kujiandaa kila siku.

Yaani uwe kama mchezaji wa akiba anayepiga “Jaramba” akisubiri kuingizwa acheze.

Fursa yako iko njiani, cheo chako kinakuja, dili linakaribia, connection inasogea.

,

Ila swali ni “Umejiandaa?”

.

Inatagemea unataka nini, inawezekana ni kujiandaa kitabia, kuongezea ujuzi au kujiandaa kipesa n.k.

.

USISUBIRI SIKU YAKO IJE NDIO UANZE KUJIANDAA, ANZA MAPEMA.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment