Hivi Unajua Kuwa Miaka Ya Watu Huwa Inaliwa?…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Yaani, kuna vitu/mambo yanatokea kwenye maisha ya mtu.

Na anajikuta amepoteza muda mwingi sana.

Na imemsababishia kushindwa kupiga hatua.

Moja ya vitu vinavyokula miaka ya wengi ni MAHUSIANO.

Ndio, yaani kuna watu miaka yao imeliwa kwa kuwa kwenye mahusiano ambayo yamewapotezea vitu vingi.

Kuna watu ambao waliwekeza kwenye mahusiano na watu kiwango kikubwa sana.

Na mwisho amejikuta mahusiano yameishia njiani.

Mbaya zaidi, kuna watu ambao wanakuja kwenye mahusiano na wewe kimkakati.

Wakilenga KUKUPOTEZEA MUDA na KUFAIDIKA Kisha wanaondoka.

Ukijikuta umetokewa na jambo hili…

Kwanza hakikisha huo ukurasa unaufunga haraka sana.

Usiendelee kulalamika na kulia kila siku.

Pili, jitahidi kuanza maisha mapya haraka kadiri unavyoweza.

Kuna maisha baada ya maumivu, usihitimishe kuwa ndio umefika mwisho.

Mbele kuna Furaha inakusubiri.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment