Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mtu mmoja alishawahi Kusema “Ni bora kwenye maisha uangalie nyuma na useme,siamini kama nilifanya hili;kuliko uangalie nyuma na useme natamani ningelifanya lile”(It’s better to look back on life and say, ‘I can’t believe I did that,’ than to look back and say, ‘I wish I did that).
.
Kila siku unakabiliwa na fursa na changamoto za kukutengenezea moja ya sentensi hizi ambazo lazima utasema mojawapo itakapofika kesho.Aidha UTAJIVUNIA kuwaULIFANYA ama UTAJUTIA kuwa HAUKUFANYA.
.
Kuna jambo ambalo LINAKUSUMBUA SANA kufanya maamuzi yake na kuna uamuzi wa aina mbili tu:UCHUKUE hatua ambayo kesho utajivunia ama uache kufanya ili kesho ujutie.Kila siku umekuwa ukighairisha kwa Hofu ya MAUMIVU na gharama;Ila Kumbuka kuna siku utatafakari na aidha utajutia ama utajivunia.
.
Leo utakutana na Kitu kitakachokuweka Njia panda KIMAAMUZI na utalazimika uchague KUFANYA hata kama hautaeleweka na itakupelekea kupata maumivu ya Muda mfupi ila FURAHA YA KUDUMU ama UKWEPE KUFANYA ili ufurahi kwa MUDA MFUPI ila ubakie na MAJUTO YA KUDUMU.
.
Je,ikifika kesho unataka ujivunie kwa kuwa JASIRI kufanya kitu leo au UTAJUTIA kwa kuwa MUOGA na kitochukua hatua?.
JIVIKE UJASIRI na TENGENEZA kesho YAKO kwa KUCHUKUA HATUA LEO!
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.