Sio lazima kila mtu atoe maoni na ASIFIE unachofanya…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna watu wengi sana ambao wanakata tamaa kwa sababu wanaona kama wanachofanya hakuna anayekiona ama kukisifia.

Haujaja duniani kumuhudumia kila mtu.

Kuna watu maalumu ambao Mungu amekusudia waguswe kupitia maisha yako na kile unachokifanya.

Moja ya stress kubwa kwenye maisha ni pale unapotaka kila mtu aone unachofanya, utapata ugonjwa wa moyo bure.

Katika historia ya dunia hakuna aliyewahi kusifiwa na kila mtu hata kama alifanya kitu kizuri sana.

Unatakiwa kufanya nini?

1. Tambua watu ambao unataka kugusa maisha yao.

Weka nguvu zako kwenye kuwafikia na kuwahudumia kwa uaminifu.

Kadiri unavyogusa wale uliotumwa kwao, ndivyo ambavyo utajisikia utoshelevu wa moyo na ndivyo Mungu atakavyopanua wigo wako.

“Focus” maana yake ni kufanya ulichoitiwa bila kukatishwa tamaa na wasiokitambua unachofanya.

Ni kuendelea kufanya hata kama hakuna anayelike au kucomment😂.

Kuna wengi utakutana nao baadae watakuambia…

…“Yaani umekuwa ukinisaidia tangu miaka 3 iliyopita”, na unakuta hawajawahi kukuambia.

ENDELEA KUFANYA!

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment