Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna tabia mbili ukiwa nazo zinaweza kukupa stress sana…
…na kukuharibia mahusiano na watu ambao wangeweza kuwa msaada kwenye maisha yako.
Tabia ya kwanza ni kuwa na wivu wengine wanapoinuliwa.
Hii ukiiendekeza itakutesa sana.
Kwenye maisha yako, kila wakati lazima kuna watu watang’ara zaidi yako.
Lazima kuna watu watainuliwa kwenye maeneo yao zaidi yako…
…wapo ambao watasifiwa tu kuliko wewe.
Ukiwa mtu ambaye unaumia wengine waking’ara, itakutesa sana.
Utaishia kuwa mtu wa majungu na kuwasema vibaya wengine ambayo haitakusaidia.
Jifunze kukubali uwezo wa wengine.
Learn to Appreciate, Learn to Celebrate Others.
Jambo lingine ni kufanya vitu ili kushindana na wengine.
Kuna watu wengi wamepoteza mwelekeo wa maisha yao…
…kwa sababu ya kutaka kuprove kwa wengine kuwa wako juu zaidi yao.
Kuna watu wanatumia gharama kubwa sana na kupoteza rasilimali zao…
…ili tu kuonesha kuwa wako juu zaidi ya wengine.
Usisahau kuwa ni hasara kubwa kwenye maisha yako kushindana na mtu ambaye yuko kwenye wito wake.
Yaani, hata siku moja mwanadamu hawezi kushindana kuogelea na samaki, atajichosha tu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.