Aliyoyasema Trump baada ya mkutano wake na Rais Zelensky

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Trump

Muda mfupi uliopita, Donald Trump alizungumza kwenye Fox News, akitoa maoni yake kwa mara ya kwanza tangu rais wa Marekani na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky kukutana katika Ikulu ya White house Jumatatu, pamoja na washirika wengine wa Ulaya.

Trump anasema anapanga mkutano kati ya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin na Zelensky ambao hautamjumuisha hapo awali.

“Ikiwa hiyo itafanikiwa, basi nitakwenda na kuufunga,” anasema.

Anasema anatumai Zelensky “ataonesha kubadilika” katika mazungumzo.

Trump anasisitiza kuwa wanajeshi wa Marekani hawatakuwa Ukraine kama sehemu ya dhamana ya usalama inayotafutwa na Kyiv.

Mataifa ya Ulaya kwa upande mwingine yanaweza kuwa na wanajeshi nchini Ukraine kama sehemu ya makubaliano, Trump anasema.

Pia anasema washirika wa Ukraine na Nato wanapaswa kuachana na juhudi za kuifanya Ukraine ijiunge na muungano wa usalama na kurejesha Crimea, ambayo Urusi iliikalia mwaka 2014.

“Mambo yote mawili hayawezekani,” anasema.

Anasema mazungumzo yake na Putin jana haikufanyika mbele ya washirika wa Ulaya na Nato. “Nilidhani hiyo itakuwa ni dharau kwa Rais Putin,” anasema.

Trump asema Zelensky anahitaji kuwa tayari kubadilika na tabia ya Putin ‘itakua nzuri’

Akizungumza moja kwa moja kwenye televisheni ya Marekani, Fox News Rais wa Marekani Donald Trump amezungumzia uwezekano wa mkutano wa pande tatu utakaowahusisha Vladimir Putin na Volodymyr Zelensky.

Anasema alimpigia simu Putin jana na anatumai kuwa tabia ya kiongozi huyo wa Urusi “itakuwa nzuri”.

Ikiwa sivyo, “hali itakuwa mbaya”, Trump anaongeza.

Trump anasema anatumai Zelensky “atafanya kile anachopaswa kufanya”, lakini anasisitiza kwamba anahitaji “kubadilika” katika mazungumzo pia.

Trump anaongeza kuwa hatasema Zelensky na Putin watakuwa “marafiki wa karibu”-

Wapatanishi wasubiri majibu ya Israel kuhusu pendekezo jipya la kusitisha mapigano Gaza

Familia za mateka na wafuasi wao wanataka serikali ya Israel ikubaliane makubaliano ya kumaliza vita na kuwarudisha nyumbani wote

Wapatanishi wa Kiarabu wanasubiri jibu rasmi kutoka kwa Israel baada ya Hamas kusema imekubali pendekezo jipya la kusitishwa kwa mapigano Gaza na kuachiliwa kwa mateka.

Mpango huo uliwasilishwa na Qatar na Misri, ambazo zinajaribu kuepusha mashambulizi mapya ya Israel ya kuikalia Gaza kikamilifu.

Qatar ilisema “inakaribia kufanana” na pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano kwa siku 60, ambapo karibu nusu ya mateka 50 wanaoshikiliwa Gaza, 20 kati yao wanaaminika kuwa hai, watakabidhiwa na pande hizo mbili zitafanya mazungumzo ya usitishaji vita wa kudumu na kurejea kwa wengine.

Katika siku za hivi karibuni, serikali ya Israel imesema haitakubali tena makubaliano ya sehemu, makubaliano ya kina tu ambayo yatawafanya mateka wote waachiliwe.

Vyombo vya habari vya ndani vilimnukuu afisa mkuu wa Israel akisema: “Msimamo wa Israel haujabadilika, kuachiliwa kwa mateka wote na kutimiza masharti mengine yaliyoainishwa ya kumaliza vita.”

Baadaye wiki hii, baraza la mawaziri la Israel linatazamiwa kuidhinisha mpango wa jeshi wa kuukalia kwa mabavu mji wa Gaza, ambapo mashambulizi ya Israel tayari yamewafanya maelfu ya watu kukimbia.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alitangaza nia ya Israel ya kuiteka Gaza yote, ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo wakazi wake wengi milioni 2.1 Wapalestina wametafuta hifadhi, baada ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Hamas juu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuvunjika mwezi uliopita.

Serikali ya Burkina Faso yamfukuza afisa mkuu wa UN kutokana na ripoti ya haki za watoto

Carol Flore-Smereczniak

Utawala wa Burkina Faso umemfukuza afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa katika taifa hilo la Afrika Magharibi kutokana na ripoti kuhusu watoto walionaswa katika mzozo wa wanajihadi.

Carol Flore-Smereczniak alitangazwa kuwa “mtu asiyekubalika” kwa sababu ya jukumu lake katika kuandaa ripoti iliyotoka Machi.

Ukijumuisha kipindi cha miaka miwili, utafiti huo ulieleza kwa kina zaidi ya kesi 2,000 za kuripotiwa kuajiriwa kwa watoto, mauaji, unyanyasaji wa kingono na unyanyasaji, ukiwalaumu waasi wa Kiislamu, wanajeshi wa serikali na vikosi vya ulinzi vya raia.

Serikali ya kijeshi, iliyoingia madarakani Septemba 2022 na ikiongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré, ilisema haikushauriwa na UN, ikisema ripoti hiyo ina madai yasiyo na msingi.

Haikutaja nyaraka zozote “au maamuzi ya mahakama kuunga mkono madai ya kesi za ukiukaji wa haki dhidi ya watoto zinazohusishwa na wapiganaji hodari wa Burkinabe”, taarifa ya serikali ilisema.

Tangu mwaka wa 2015, waasi wa kijihadi wenye mafungamano na al-Qaeda na kundi la Islamic State wameendesha uasi ambao umeua maelfu ya watu na kuwalazimisha mamilioni kukimbia makazi yao.

Imesababisha kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, na mapinduzi mawili ya kijeshi mwaka wa 2022.

Capt Traoré alichukua mamlaka akiahidi kukabiliana na hali mbaya ya usalama ndani ya “miezi miwili hadi mitatu”.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment