Muungano wa Nchi za Kiarabu walaani matamshi ya Netanyahu kuhusu ‘Maono makubwa ya Israel’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anahisi yuko kwenye “ujumbe wa kihistoria na kiroho,” na “anajitolea sana” kwa maono ya Israeli makubwa, ambayo yanajumuisha maeneo ya Palestina, “na labda pia sehemu za Jordan na Misri,” kulingana na The Times of Israel

Muungano wa Nchi za Kiarabu walaani matamshi ya Netanyahu kuhusu ‘Maono makubwa ya Israel’

h

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anahisi yuko kwenye “ujumbe wa kihistoria na kiroho,” na “anajitolea sana” kwa maono ya Israeli makubwa, ambayo yanajumuisha maeneo ya Palestina, “na labda pia sehemu za Jordan na Misri,” kulingana na The Times of Israel.

Gazeti hilo liliripoti kwamba Sharon Gal, mhojiwaji wa idhaa ya Israel i24, ambaye kwa muda mfupi alikuwa mwanachama wa mrengo wa kulia wa Knesset, alimpa Netanyahu hirizi katika mfumo wa “ramani ya Nchi ya Ahadi.” Alipoulizwa jinsi alivyojitambulisha na “maono” haya ya Israeli makubwa, Netanyahu alijibu, “Hakika.”

Neno “Israeli Kubwa” lilitumika baada ya Vita vya Siku Sita mnamo Juni 1967, ambavyo pia vilijulikana kama “Naksa,” kurejelea Israeli na maeneo iliyokuwa inayamiliki wakati huo, ambayo ni pamoja na Jerusalem Mashariki, Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza, Rasi ya Sinai, na Milima ya Golan.

Gazeti la Israel lilibainisha kuwa “baadhi ya Wazayuni wa awali walitumia maneno haya ku husiana na Israel ya sasa, Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Jordan.”

Wakati wa mahojiano hayo , Netanyahu aliulizwa jinsi alivyohisi alikuwa kwenye harakati kwa niaba ya watu wa Kiyahudi. Alijibu, “Mimi niko kwenye ujumbe wa kizazi. Kuna vizazi vya Wayahudi ambavyo vimeota kuja hapa, na vizazi vya Wayahudi vitakuja baada yetu.

Viongozi wa Ulaya wana matumaini baada ya kuwasiliana na Trump kabla ya mkutano wa kilele wa Putin

g
Maelezo ya picha,Friedrich Merz wa Ujerumani alimkaribisha Rais Zelensky mjini Munich siku ya Jumatano

Viongozi wa Ulaya wameonekana kuwa na matumaini makubwa baada ya kufanya mkutano wa kawaida na Donald Trump siku ya Jumatano, siku mbili kabla ya kukutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin huko Alaska kujadili kumaliza vita nchini Ukraine.

Trump aliripotiwa kuwaambia viongozi hao wa Ulaya kwamba lengo lake la mkutano huo ni kupata usitishaji wa mapigano kati ya Moscow na Kyiv.

Pia alikubali kwamba masuala yoyote ya kimaeneo yanapaswa kuamuliwa kwa kuhusika kwa Volodymyr Zelensky, na kwamba dhamana ya usalama inapaswa kuwa sehemu ya mpango huo, kwa mujibu wa Emmanuel Macron wa Ufaransa.

Kuzungumza na Trump kumempa Zelensky fursa ya “kufafanua nia yake” na kuipa Ulaya nafasi ya “kueleza matarajio yetu,” Macron alisema.

Trump na Makamu wa Rais JD Vance walizungumza na viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Finland na Poland pamoja na mkuu wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na mkuu wa Nato Mark Rutte.

Ulaya imetengwa katika mkutano wa kilele ulioandaliwa kwa haraka huko Alaska na simu yao Jumatano ilikuwa jaribio la mwisho la kuweka masilahi ya Ukraine na usalama wa bara hilo mbele ya mawazo ya Trump.

Marekani yaliwekea vikwazo kundi la PARECO-FF linalofanya kazi na Kinshasa

f
Maelezo ya picha,Mpiganaji wa PARECO huko Nyamilima, Kivu Kaskazini, mwaka wa 2008.

Marekani imeliwekea vikwazo kundi lenye silaha nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo linalofanya kazi na serikali ya Kinshasa, chama cha ushirika cha uchimbaji madini nchini humo, na makampuni mawili ya Hong Kong, ikiywatuhumu kuchangia ukosefu wa usalama nchini DRC na uchimbaji madini kinyume cha sheria.

Wizara ya fedha ya Marekani inasema inalenga moja ya makundi yanayofanya kazi na serikali ya DRC, PARECO-FF (Coalition des Patriotes Résistants Congolais-Force de Frappe), ikilishutumu kwa “kuendesha miradi haramu ya uchimbaji madini na ushuru huko Rubaya”.

Kundi hilo, linaloundwa zaidi na Wahutu kutoka DRC, lilidhibiti migodi katika eneo la Rubaya – ambayo ina madini ya thamani muhimu kwa sekta ya teknolojia, ikiwa ni pamoja na simu za mkononi -kuanzia mwaka 2022 hadi mapema 2024, kulingana na Marekani.

John K. Hurley, Naibu Waziri wa fedha wa Marekani, alisema kuwa “madini ya migogoro yanaua raia wa Congo, kuchochea rushwa, na kukvuruga biashara halali za kuwekeza nchini DRC.”

“Wizara ya fedha haitasita kuchukua hatua dhidi ya mashirika ambayo yanainyima Marekani na marafiki zetu kupata madini ya thamani ambayo ni muhimu kwa usalama wa taifa letu,” alisema.

Ni madai hayo ‘uongo, dharau, kashfa na uchochezi’: Melania Trump atishia kumshtaki Hunter Biden kuhusiana na madai ya Epstein

h

Mke wa Rais Melania Trump ametishia kumshtaki Hunter Biden kwa zaidi ya $1bn baada ya kudai kuwa alitambulishwa kwa mumewe na mkosaji wa ngono Jeffrey Epstein.

Mawakili wanaofanya kazi kwa niaba ya mke wa rais, ambaye aliolewa na Rais wa Marekani Donald Trump mwaka wa 2005, wameelezea madai hayo kuwa ya “uongo, dharau, kashfa na uchochezi”.

Biden, ambaye ni mtoto wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, alitoa maoni hayo wakati wa mahojiano mapema mwezi huu, ambapo aliukosoa vikali uhusiano wa zamani wa rais huyo na Epstein.

Donald Trump alikuwa rafiki wa Epstein, lakini amesema wawili hao walitofautiana mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwasababu mfadhili huyo alikuwa amewawinda kiharamu wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi kwenye saluni na urembo (spa) katika klabu ya gofu ya Trump ya Florida.

Barua kutoka kwa mawakili wa mke wa rais na iliyotumwa kwa wakili wa Hunter Biden inamtaka abatilishe madai hayo na kuomba radhi, au atachukuliwa hatua za kisheria kwa “fidia ya zaidi ya $1bn”.

Inasema kuwa mke wa rais amepata “madhara makubwa ya kifedha na sifa” kwa sababu ya madai aliyorudia.

Pia inamtuhumu mtoto huyo mdogo wa kiume wa Biden kwa kuwa na “historia kubwa ya kufanya biashara kwa majina ya wengine”

Spurs yalaani ubaguzi wa rangi dhidi ya Mathys Tel

g
Maelezo ya picha,Tel aliingia kama kiungo mbadala katika dakika ya 79

Tottenham wamesema “wamechukizwa” na unyanyasaji wa kibaguzi aliopokea mshambuliaji Mathys Tel kufuatia kushindwa kwao na Paris St-Germain kwenye michuano ya Uefa Super Cup.

Klabu hiyo, ambayo ilishindwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kuongoza kwa mabao mawili kwa moja, ilisema watu waliotuma ujumbe wa matusi kwa Tel kwenye mitandao ya kijamii “si chochote ila waoga”.

Tel, 20, aliingia kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 79 na alikuwa mmoja wa wachezaji wawili wa Spurs ambao walishindwa kufunga bao kwenye mikwaju ya penalti.

“Mathys alionyesha ujasiri wa kusonga mbele , lakini wale wanaomnyanyasa si chochote ila waoga – wanaojificha nyuma ya majina ya watumiaji na wasifu ambao haukujulikana kudhihirisha maoni yao ya kuchukiza,” Tottenham ilisema.

“Tutashirikiana na mamlaka na mitandao ya kijamii kuchukua hatua kali iwezekanavyo dhidi ya mtu yeyote ambaye tunaweza kumtambua.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment