Kutumia Simu vizuri….

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ni kawaida kujikuta unatumia simu kama njia ya kumtafuta mtu ambaye unamuhitaji sana.

Hata hivyo kuna mambo 3 ya msingi ya kuzingatia ili usiwe kero kwa huyo mtu na ukafanya asikupe nafasi:

1. Usipige Mfululizo Wa Simu Nyingi Kwa Wakati Mmoja.

Kuna watu wanaamini wakimpigia mtu simu mara nyingi ndio itapokelewa, badala yake utaonekana msumbufu.

Jitahidi usipige zaidi ya mara mbili mfululizo.

Kuna watu wanapiga hata mara kumi hadi simu ya anayempigia inaisha chaji, anakuta missed calls 10.

Hii haitakusaidia, itafanya akublock au asipokee tena na anakusave msumbufu.

Ukiona mtu hapokei inawezekana yuko kwenye kikao, amesahau simu mahali, hayuko kwenye mood n.k

Tuma meseji itasaidia zaidi kuliko kuendelea kupiga mfululizo kama viel unamdai.

2. Jitambulishe Na Muombe Kuongea Naye.

Usipige simu kwa mtu halafu unaanza kumuuliza “Naongea na Fulani?” – Sio sawa.

Jitambulishe kwanza wewe kwa ufasaha na eleza kushukuru / kufurahi amepokea simu yako.

Baada ya hapo omba muda wa kuongea naye – “Naomba dakika tatu za kuzungumza na wewe tafadhali “.

Hii ni kumuonyesha unajali muda wake na vipaumbele vyake.

Kama hayuko sehemu nzuri sana ya kuongea atakuambia muda mzuri wa kumpigia na kama yuko sehemu nzuri atakuambia endelea.

3. Nenda Moja Kwa Moja Kwenye Point.

Acha stori ambazo zitapoteza muda zaidi.

Jikite kwenye hoja kabisa.

Ni vizuri watu wa namna hii ujiandae aidha kwa kuandika mahali au kupanga point zako vizuri na kufanyia mazoezi kabla haujapiga simu…

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment