Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hivi unajua kuwa unaweza ukafahamiana na watu wengi ila hauna mahusiano nao?
Kwenye maisha, usikusanye watu tu, jenga mahusiano.
Usijivunie kujuana na watu wengi, bali jenga urafiki wa dhati.
Umeshawaza leo ikitokea bahati mbaya ghafla ukaondoka duniani…
…una mtu ambaye anaweza kujitolea kutunza watoto wako kwa upendo hadi watakapoweza kujitegemea.
Au watabakia wanateseka na hawatapa msaada wowote kutoka kwa wanaoonekana rafiki zako wa karibu?
Hivi, Una mtu ukimpigia simu anaweza kuacha kila kitu usiku na akajitoa kuja kukusaidia?
Ikitokea umeenda jela kwa kosa la aibu bado kuna mtu atakutembelea na hataona aibu kuwaambia watu kuwa wewe ni rafiki yake?
Ukishindwa uchaguzi bado atakuwa na wewe na ataendelea kukutafuta?
Ukipoteza utajiri nani ataendelea kuwa karibu na wewe?
Kwa mfano leo ukipoteza cheo chako…
…unaweza kutaja ni watu wangapi wataendelea kukutafuta kila siku.
Moja ya hatari ya ulimwengu wa sasa, ni kujikuta unawajua watu wengi na unajulikana na wengi… ..ila rafiki zako wa ukweli ni wachache.
Leo, anza siku kwa kutafakari hazina uliyonayo ya watu wa dhati na hakikisha, unapoendelea kufahamiana… …na watu unatumia pia muda wako kujenga mahusiano yenye thamani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.