Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeripoti umatano asubuhi kwamba ndege zisizo na rubani 46 za Ukraine zilidunguliwa usiku kucha katika maeneo sita ya Urusi, ikiwa ni pamoja na Crimea , jimbo lililotwaliwa..
Wizara hiyo inasema kuwa ndege zisizo na rubani 15 zilidunguliwa kwenye mpaka wa eneo la Bryansk, 11 juu ya Volgograd, saba juu ya Rostov, na tano juu ya Krasnodar Krai. Ndege zisizo na rubani zilizobaki, kulingana na taarifa hiyo, zilipigwa risasi juu ya mikoa ya Belgorod na Voronezh, na pia juu ya Crimea na Bahari ya Azov.
Huko Slavyansk-na-Kubani huko Krasnodar Krai, uchafu wa UAV ulianguka kwenye eneo la kiwanda cha kusafisha mafuta, na gari likaungua moto, mamlaka ilisema.
Kikosi kazi cha kikanda pia kiliripoti kwamba vipande vya ndege zisizo na rubani vilianguka katika mazingira manne ya makazi na maeneo ya karibu.
Huko Volgograd, uchafu wa droni ulianguka juu ya paa la jengo la makazi la orofa 16, Gavana Andrei Bocharov aliripoti .
Shughuli za uokoaji zinaendelea kuwaokoa watu 22 waliofukiwa kwenye mgodi wa madini Tanzania

Huduma za uokoaji zinaendelea kuwaokoa takribani watu 22 waliofukiwa na kifusi, katika machimbo ya dhahabu ya Nyandolwa, Shinyanga Tanzania
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema tukio hilo limetokea wakati mafundi wakiufanyia ukarabati mgodi huo na kwamba mpaka jana usiku watu watatu walikuwa wameokolewa.
Mboni Mhita amesema wanachokifanya sasa ni kutengeneza njia ambayo ni salama zaidi kuweza kuwafikia. ‘’Changamoto iliyopo ni kwamba eneo lina mawe sana sio eneo ambalo ni teketeke. Ni toauti na maeneo ya uchimbaji ambayo ni teketeke’’, amesema.
Ametoa wito wa ukarabati wa mashimo ya machimbo ya madini kabla ya shughuli za uzalishaji kuanza.
Matukio ya wachimba madini kunaswa katika machimbo si mageni nchini Tanzania kwasababu ya vifaa duni vya uchimbaji wanavyovitumia.
CHAN 2024: Kenya, Zambia na Morocco zapigwa faini ya maelfu ya dola kwa kukiuka sheria za CAF

Bodi ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) imeitoza Kenya faini ya USD 50,000 baada ya kuipata na hatia ya ‘’ukiukaji mwingi wa usalama na usalama” kwenye Uwanja wa Kasarani wakati wa mechi ya CAN 2024 dhidi ya Morocco.
Aidha CAF imeionya Kenya kuwa kushindwa kushindwa kutimiza matakwa ya usalama na kunaweza kusababisha kuhamishwa kwa mechi za Timu ya Taifa ya Kenya hadi uwanja mbadala.
Kenya ilishauriwa kuongeza hatua za kudhibiti usalama kwa kupeleka wafanyakazi wa kutosha ndani ya eneo la uwanja na pia kuzingatia kufungwa kwa barabara siku za mechi.
Hii ni baada ya Bodi ya Nidhamu ya CAF kulishtaki Shirikisho la Soka la Kenya (“FKF”) kwa ukiukaji mwingi wa usalama wakati wa mechi ya Kenya ya michuano ya Mataifa ya Afrika (“CHAN”) dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi, Kasarani.
Bodi hiyo pia ililipata shirikisho la soka la Morocco Fédération Royale Marocaine de Football (“FRMF”) na hatia ya kuwa na mwenendo usiofaa wa wachezaji wake wakati wa mechi ya Morocco ya CAF michuano ya Mataifa ya Afrika (“CHAN”) dhidi ya Kenya na kuitoza faini ya USD 5,000 , ambapo USD 2,500 zitasimamishwa kwa masharti kwamba hakuna kosa kama hilo litakalotekelezwa katika kipindi kilichosalia cha CHAN 2024.
Zambia pia imetozwa faini ya USD 5,000 kwa kukiuka Kanuni za Vyombo vya Habari vya CAF wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwa Zambia ilishindwa kuwasilisha kocha mkuu katika mkutano wa lazima wa Wanahabari Siku ya Mechi-1 kabla uliofanyika kabla ya ya mechi yao dhidi ya Jemuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
Faini hizo zitalipwa ndani ya siku 60 baada ya taarifa ya uamuzi huu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.