Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Habari kaka mimi ni mdada wa miaka 31 nimekaa na mume wangu miaka 10 sasa tumejaliwa kupata watoto wawili wa kike mmoja miaka minane mwingine miaka minne kusudi la kuja kwako nikuhusu ndoa
Mume wangu mimi ni mtumishi wa serikali ni askari jeshi tulichukuana bila kufunga ndoa japo kuna taratibu za kikazi zilimuhitaji kuwa na ndoa ndipo tulipoamua kwenda kutafuta vyeti vya ndoa ilikuweza kupeleka kazini tumekaa miaka yoote mimi nilikuwa mwajiliwa wa kampuni fulani ndipo alipoamua kuniachisha kazi nakunifungulia biashara wakati huo tukiwa tunatambulika sehemu zoote mbili yaani kwao kanitambulisha kwetu nikamtambulisha na akatoa pesa ya kishika uchumba akidai ataenda kutoa mahali
Siku zimeenda wazazi wangu wakafariki nikabaki na wazazi walezi nikamwambia basi twende ukatoe mahali akawa anasema anajipanga tumekaa huku mimi nikiendelea kufanya biashara alinifungulia duka la mahitaji ya nyumbani nilianza na mtaji mdogo hatimae ukakua nikaja nikajifungua hivyo nikamuomba siku hajaingia kazini awe ananishikia alikubali na kufanya hivyo lakini matokeo yake alikuja kuanza kukopesha staff wenzake na wakawa hawawezi kulipa tena akapata mwanamke pale mtaani akawa anamhonga vitu vya dukani
Nilivyogundua na biashara ikalega kabisa ukimwambia anakuwa mkali basi nikamshawishi nikamwambia tuliuze akakubali nikatafuta mteja nikauza kwa heshima nikaja nikamwambia na nikamuonyesha pesa nilizouza kwakua nilikuwa nakachanga bado basi nikaona nikae nyumbani kwanza nilee kakikua nitatafuta kitu cha kufanya nikaona pesa haitunziki nikamwambia mume wangu basi tukatafute kiwanja hii pesa tununue then nikitaka kuanza biashara tutajichanga tukanunua kiwanja basi nikalea mtoto amekua nikamwambia mume wangu naomba sasa tufungue biashara tena akakubali na akanipa pesa nikafungua tena ila kile kitendo cha kufungua biashara mume wangu alibadilika mshahara ukawa hauonekani na akataka duka lihusike kwa kila kitu na huku mtaji ulikuwa kidogo akawa mtu wa magenge ,anacheza makamali akiishiwa hela anakopa mpaka kausha damu za huko mtaani akaniachaniza majukumu yoote mpaka duka likaisha kabisa ikabidi niende ofisini kwake kutoa malalamishi tukashauliwa tukarudi nyumbani nakuendelea
Sasa biashara imefungwa mtaji ukaisha na maisha yakawa bado magumu tulikuwa tumepanga uraiani hadi tukarudishwa nyumba za kazini kwake na sasa tumekuwa tukiedelea kuishi ada za watoto hawezi kumeki ukifika wakati wa ada anakopa Bank analipia watoto mwaka mzima kitu kinachonishinda kwake kwa sasa hashauliki na kibaya zaidi tukigombana ananichonganisha na ndugu zake napigiwa simu na mamaaake natukanwa na mawifi nilisha jaribu kuondoka akanililia na kuniomba msamaha nirudi nikakubali nimerudi lakini tabia inaendelea
Kuna kipindi niliwahi kwenda kwa mama mkwe kumuona nikakuta ana maisha magumu niliumia nikatoa pesa kumnunuli vitu kwa upendo na nikaja kumwambia mwanae ili aweze kumkumbuka mzazi wake lakini alimpigia mamaake baada yakugombana na kumwambia namsimanga yule mpaka akawa ananiambia subiri nipokee mchezo nikurudishie pesa zako inshort huyu Mama mkwe hajamlea mume wangu aliwatelekeza amekuja kumjua akiwa kazini hivyo mume wangu alikuwa na Baba na Mama wa kambo ila huyo Baba ni marehemu sasa naomba ushauri kuondoka natamani hata saa hizi but nikiangalia watoto wangu roho inaniuma saana na nikisema niondoke nao bado sijajipanga naomba ushauri jamani mwenzenu najikaza huku nateketea msaada
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.